Will Smith huenda akaitosa Independent Day Part 2
http://habari5.blogspot.com/2014/02/will-smith-huenda-akaitosa-independent.html
HUENDA staa wa filamu ya Independence Day Will Smith asirejee tena kwenye mwendelezo wa utengenezaji wa filamu hiyo.
Filamu hizo zinazotengenezwa na kampuni kongwe ya utengenezaji filamu ya 20th Century Fox inatarajia kutoa filamu nyingine mwaka 2016.
Kwa mujibu wa mtandao wa The Wrap wa Marekani unaojishughulisha na habari za wasanii na watu maarufu ulibainisha kuwa Smith amekuwa akisita kuelezea ushiriki wake katika filamu hiyo kwa mwaka 2016.
Filamu ya Independence Day ni moja kati ya filamu ambazo zilimtambulisha Wil Smith rasmi katika ulimwengu wa filamu ambapo alikuwa akiigiza kama rubani wa ndege kapteni Steven Hiller.
Watayarishaji wa filamu hiyo Roland Emmerich na Dean Devlin wamekuwa wakiendelea na jitihada zao za kufanikisha toleo la pili la filamu hiyo iliyoandikwa na James Vanderbilt.
Katika mwongozo huo wa filamu Will Smith ametajwa kuwa ni mmoja kati ya walengwa wakuu watakaoshirikishwa kwenye toleo hilo la pili na pia kuna mtu mwengine nae amelengwa.
Kusitasita kwa Smith kusema kama atashiriki au la kumezua mjadala kuwa anaweza asiendelee na filamu ya pili ya Independence Day.
Kuna mwigizaji mwengine aitwaye Jordan ambae anaonekana kuwa anaweza kuchukua nafasi hiyo ya Will Smith.
==================================