Michael Jordana apata mapacha wa kike kwa mkewe wa sasa aliewahikuwa mwanamitindo
http://habari5.blogspot.com/2014/02/michael-jordana-apata-mapacha-wa-kike.html
ALIEKUWA mchezaji gwiji wa mpira wa kikapu wa ligi ya mchezo huo Marekani, NBA Michael Jordan amepata watoto mapacha.
Jordan ambae alitengana na mkewe na kufunga ndoa na mwanamke mwengine Yvette wamepata watoto hao mapema wiki hii.
Watoto hao wa kike mmoja anaitwa Victoria na mwenzake anaitwa Yabel.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa hizo Estee Portnoy ambae ni msemaji wa timu ya Charlotte Bobcats inayomilikiwa na Jordan alisema kuwa mkewe Jordan na familia nzima kwa sasa wanaendelea vema.
Jordan ambae kwa sasa ana miaka 51 alifunga ndoa na mwanamitindo wa zamani Yvette Prieto mwaka jana Florida.
Jordan anao watoto watano wengine ambao ni Jeffrey, Michael, Marcus ,James na Jasmine aliwapata kwa mkewe wa kwanza Juanita Vanoy.
Jordan ni mmoja kati ya waasisi wakubwa wa mchezo wa kikapu na aliipatia umaarufu timu yake ya Chigaco.