Yanga kazi ni moja tu Comoro


YANGA leo huenda ikaendeleza ubabe wake wa mabao ya ushindi kwa timu ya Komorozine de Domoni ya Anjuan Visiwa vya Comoro katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mchezo huo utachezwa mjini Mitsamihuli kwenye uwanja wa Sheikh Said Mohamed International kuanzia majira ya 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Mashariki.


Yanga ambayo katika mchezo wake wa awali ilishinda kwa 7-0 dhidi ya timu hiyo na leo katika mchezo wake wa ugenini inajiamini kuwa ipo katika mazingira ya kupata ushindi zaidi.


Yanga tangia awali ilikuwa katika hali ya kuwa itawashinda wacomoro hao na kukutana na timu ya Al Hillar ya Misri na hiyo ni kufuatia hatua yake ya kuuza haki zake za Tv kwa timu hiyo kabla hata ya kucheza na Wacomoro.


Timu hiyo ikiwa chini ya kocha wake mkuu wa Hans Van der Pluijm juzi na jana ilikuwa ikifanya mazoezi mepesi katika uwanja mdogo wa hotel ya Retaj iliyofikia.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye tovuti ya Yanga ilisema kuwa timu hiyo jana ilitumia muda wake mwingi kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sheikh Said ambao utatumiwa kwa mchezo huo.


Taarifa hiyo ilisema kuwa lengo likiwa kuuzoea uwanja huo wachezaji kwa sasa wapo katika hali nzuri ya kimchezi na wanaweza kuimudu timu leo.


Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van der Pluijm alisema anashukuru kikosi chake kipo vizuri kuelekea mchezo huo na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja hivyo anapata fursa ya kuchagua amtumie nani katika mchezo huo.


Akiongelea wapinzani timu ya Komorozine de Domoni amesema hawajaidharaua mechi hiyo kama watu wengi wanavyofikiria, kikubwa amewaandaa vijana wake waeze kufanya vizuri na kupata ushindi.


"Kwangu mie hakuna mechi ndogo wala mchezo wa kirafiki naichukulia hii kama mechi muhimu kwa Yanga" alisema Hans.


Young Africans itashuka dimbani kucheza mchezo huo wa marudiano ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 7-0 iliyoupata katika mchezo wa awali uliofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.


Katika kikosi hicho wachezaji wa Yanga kama vile Jerryson Tetege na kipa Juma Kaseja hawatakuwapo katika mchezo huo wa leo.

Related

Sticky 1650590138816283549

Post a Comment

emo-but-icon

item