Msome mbunifu huyu wa mavazi kutoka Dodoma
http://habari5.blogspot.com/2014/02/msome-mbunifu-huyu-wa-mavazi-kutoka.html
Mbunifu kutoka D odoma |
MBUNIFU wa mavazi kutokea mkoani Dodoma Rachel Majuki amelalamikia ugumu wa biashara ya tasnia hiyo mkoani Dodoma.
Rachel aliiambia safu hii katika onesho la mavazi la Lady in Red kuwa katika Mkoa wa Dodoma wabunifu wa mvazi wenye majina makubwa ndio wanaopaa biashara zaidi.
Alisema kuwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu aliokuwa kwenye tasnia hiyo amejifunza mengi na sio kwamba hapati biashara kabisa.
Alisema kuwa biashara inapatikana lakini ni kwa muda mchache na sio kama ilivyo kwa maeneo mengine hasa katika majiji makubwa kama ya Dar es salaam, Mwanza na Arusha.
"Mkoa wetu huo wa Dodoma mbali na kuwa kuna watu mbalimbali waheshimiwa lakini sio kwamba biashara yetu hii nayo ni kubwa lakini inaonekana ni kama ndio inaanza kuchipukia"alisema Rachel.
Alisema kuwa kwa upande wake anajishughulisha na ushonaji wa nguo za
kiume na kike pamoja na nguo za asili.
Aliongeza kuwa hata hivyo kwa sasa anaona kuwa anakabiliwa na changamoto kubwa ya kujitangaza zaidi kwa kushiriki katika maonesho mbalimbali.
"Inatakiwa kwa sasa na sisi mkoani kwetu angalau kujikita zaidi katika kuandaa maonesho kama haya ya mavazi ili kujitangaza zaidi ikiwa pamoja na kushiriki kwenye maonesho ya wenzetu"alisema Rachel.