Naipongeza THT kwa kazi nzuri ya jana
http://habari5.blogspot.com/2014/02/naipongeza-tht-kwa-kazi-nzuri-ya-jana.html
Awaichi Mawala wa Zantel akizungumza na waigizaji wa kundi la Mahusiano linalorushwa na Clouds Tv na kudhaminiwa na Zantel |
Awaichi pamoja na wadau wengine wa sanaa waliokaa wakiwa na kundi la Mahusiano |
Sheba Kusaga kulia akiwa na Awaichi
Master J, Awaichi na Sheba
Sheba (kushoto) na mdau wa kundi la Mahusiano Mwinjaku |
Wasanii wa THT |
Mwijaku akimshangaa mkewe katikati (kwa mujibu wa mchezo wa Mahusiano) |
Wageni waalikwa |
Martin na Kebby |
THT ilitoa burudani safi |
Hawa ni wanafunzi wanaosoma muziki THT |
Wadau wa Habari walikuwapo kushuhudia Shafii Dauda na Mwani Nyangasa |
Marlaw aliibukia kushow love kwa THT
Arnond Madale wa Zantel (kulia) akipiga stori na wadau mbele yake ni Mwita ambe ni Media Specialist wa Lotus Pr Company |
Arnod Madale, Adam Mchomvu na Mdau |
Kazi ilikuwa nzuri |
KUNDI la uigizaji la Mahusiano linalolusha vipindi vyake kupitia Luninga ya Clouds Tv jana lilizinduliwa rasmi katika kumbi ya Escape One, Mikocheni.
Uzinduzi wa kundi hilo lililo chini ya Nyumba ya vipaji Tanzania (THT) ulienda sambamba na utayarishaji wa kipindi maalum kwa siku ya wapendanao, Valentine Day.
Hafla hiyo pia lililenga kuwakutanisha pamoja wasanii wa THT pamoja na wadau mbalimbali wa sanaa na biashara nchini.
Kundi la Mahusiano ni kundi ambalo linakuja kwa kasi kwa sasa hapa nchini hasa kutokana na mahudhui yake kuwagusa wanajamii wengi zaidi.
Uzinduzi huo ulikuwa ni sehemu ya mkakati wa THT kuendeleza sanaa za sanaa ya muziki na maigizo hapa nchini.
Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu wakiwamo wasanii wa maigizo,nyimbo pamoja na wadau wengine muhimu pia ulienda sambamba na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki kutoka THT ambao ni Barnaba,Linah,Mwasiti,Ditto,Amini na Mataaluma.
Wasanii hao waliimba nyimbo Live kwa saa tano jukwaani huku ambapo pia msanii Marlaw akiungana nao jukwaani na kuimba baadhi ya nyimbo zake chache.
Wakiwa wanaimba nyimbo zao wakiwa wamekaa kwenye viti walianza kuimba kwa zamu ambapo Mataaluma alikuwa akiongoza uimbaji huo.
Alipomaliza Mataaluma ikajan zamu ya Mwasiti alieimba nyimbo zake mbili na kisha akaimba Linah kabla ya kurudi tena kwa Mataalum.
Wasanii hao walikuwa wakiimba na kuonesha vionjo mbalimbali vya uimbaji hasa pale walipokuwa wakiimba huku wakipiga makofi.
Binafsi nikiwa kama mmoja kati ya wageni waalikwa napenda kuwapongeza THT sio tu kwa kuwa na miradi mbalimbali kwa vijana ambayo iansaidia suala zima la ajira kwa vijana hao lakini pia kwa umakini wanaouonesha katika utendaji wa kazi zao mfano mzuri ni kama yale yaliyotokea kwenye hafla hiyo.
Katika hafla hiyo binafsi niliguswa na uwezo uliooneshwa na wasanii hao katika kuimba.
Wakitajwa wasanii wa THT ni dhahiri kuwa wanakuwa wanazungumziwa wasanii wenye uwezo wa kuimba, kumudu jukwaa na mengineo kuhusiana na muziki hasa muziki wa moja kwa moja (Live music).
Hilo ndio lililojidhihirisha juzi katika onesho lao hilo baada ya kuimba live kwa zaidi ya saa nne jukwaani.
Wasanii hao walionesha umahiri sio tu katika kuimba bali pia katika suala zima la upangaji wa sauti, namna ya kupokezana kuimba pamoja na kuongeza vionjo mbalimbali katika kuimba.
Umakini kama huu ndio ambao unatakiwa kufanywa mara kwa mara na wasanii wengine wa muziki huo wa kisasa kwa hapa nchini.
Wasanii wengi hasa wa muziki wa Bongo Fleva wanashindwa kuimba muziki wa live.
Hali hiyo inatokana na uzumbe wa wasanii wenyewe kushindwa kufanya maandalizi ya kutosha hasa kwa kujifunza elimu ya muziki.
Nawachukulia wasanii hao wa THT ambao ni Linah,Barnaba,Amini,Ditto,Mataalum na Mwasiti kama wasanii mfano wa kuigwa katika kuendeleza na kuupa heshima muziki wa Bongo Fleva hapa.
Sina maana kuwa ukitoa hao hakuna wasnaii wengine wanaofanya vema la hasha, wapo wasani wengi ambao nao ni wazuri na wenye uwezo wa kuimba na kufanya live muziki lakini hata hivyo ukiangalia ni sio kwa wingi ule kama unaotakiwa au sio kwa kiwango kama hicho.
Ili kuuletea heshima muziki wa Bongo Fleva inatakiwa wasanii wanaojishugulisha na muziki huo kwanza kujiendeleza kielimu ya muziki.
Kwa kufanya hivyo inawawekea mazingira mazuri ya kuweza kuimba hata katika majukwaa ya kimataifa.
Wasanii wakijifunza kusoma nota za muziki pamoja na kutumia vifaa vya muziki wanakuwa wamejiweka katika mazingira mazuri katika soko la muziki.
Kujiendeleza kielimu ya muziki ni jukumu la wasanii husika na wanatakiwa kukumbuka kuwa ili kuupa hadhi muziki wa Bongo Fleva uheshimike kimataifa ni wao wenyewe wanatakiwa kutambua kuwa fani hiyo ni ajira rasmi na inatakiwa kusomewa.
Wasanii wasome muziki pamoja na mengineo yahusianayo na muziki kama vile, kujua biashara ya muziki, kujua namna bora ya kujitangaza kama wasanii ikiwa pamoja na kutafuta soko la kazi zao.
Pia kundi la waigizaji wanaoigiza mchezo uitwao Mahusiano unaotayarishwa na THT nalo lilitumia fursa hiyo kutangaza kazi zao katika hafla hiyo iliyofanyika katika ufukweni kwenye kumbi ya Escape One.