Sababu 10 zinaweza kuifanya Liverpool kuibuka Mabingwa msimu huu
http://habari5.blogspot.com/2014/02/sababu-10-zinaweza-kuifanya-liverpool.html
TIMU ya Liverpool inaonekana kuwa ipo katika mazingira mazuri zaidi ya kushinda taji la Ligi Kuu Uingereza hasa kwa kuwa na sababu 10 muhimu za kufanya hivyo.
Hiyo ni kufuatia timu ya Arsenal kuonekana kuwewezeka kileleni, Chelsea kutokuwa tayari huku Man City ikionekana kushindwa kujiiramisha katika nafasi yake na Manchester City ikiwa haina matumaini yoyote kabisa.
Baada ya kushinda 5-1 dhidi ya Arsenal, Liverpool imeonekana kujiamini zaidi katika nafasi nne muhimu na hivyo kuweka mazingira kushinda taji hilo.
Kwa mujibu wa jarida la Sportsmail ambalo limetaja sababu 10 za Liverpool kushinda kuwa ni katika msimu wa mwaka 1985 - 86 Liverpool ikiwa chini ya Everton kwa pointi 5 iliyokuwa ikiongoza ligi wakati huo huku ikiwa imebakiza michezo yake 13.
Lakini walijikuta wakiongeza pointi kufikia 8 huku wakiwa wamebakiza michezo 12 baada ya Everton kufungwa 2-0 na wapinzani wao kwnye uwanja wa Anfield.
Lakini kutokana na ushindi mara 11 na sare moja Liverpool ilijikuta ikitwaa ubingwa kwa tofauti ya pointi 2 dhidi ya Everton.
Sababu nyingine ni kwamba timu hii ina mchezo mwengine wanyumbani ikilinganiwa na timu za Manchester City na Chelsea wanaotakiwa kwenda Anfield, Hasa pia kam ainavyofahamika kuwa kocha wa Chelsea mwenyewe Jose Mourinho amekuwa akisema kuwa timu yake haitashinda taji hilo mwaka huu.
Liverpool inaweza kuwa haikubahatika kuifunga Manchester United kwa miaka mitano mfululizo kila walipokutana wakati huo Manchester ikiwa chini ya Sir Alex Ferguson lakini nini anaweza kumaliza histori hiyo wakikutana tena mwezi ujao wakiwa na David Moyes.
Jarida hili liliendelea kufafanua kuwa Manchester imeshafungwa na timu kama West Brom, Everton, Newcastle na Tottenham pamoja na Swansea ligi kuu Uingereza sasa ikija kukutana na Liverpool hasa kwa wakati huu si ndio inakuwa fursa ya timu hiyo ya Liverpool kujishindia.
Hivyo Liverpool ambayo kwa miaka mitano haikuwahi kushinda mechi ikiwa katika Uwanja wa Manchster United kwa miaka mitano.
Jarida hilo liliendelea kufafanua sababu nyingine za Liverpool kuwa bingwa ni pamoja na Arsenal timu iliyofungwa 5-1 na Liverpool kwa sasa ipo katika hatari ya kujikuta ikipoteza zaidi.
Timu hiyo kwa sasa imeanza kuondoka machoni mwa wapenzi wa soka kuwa kama mshindi wa kombe hilo na kuchukuliwa kama mshiriki wa kawaida anawania nafasi ya nne bora katila ligi hiyo.
Huenda mwezi ujao Arsenal inaweza kupoteza hata kwa Manchester United kwenye ligi, na Liverpool kwenye ligi kuu Uingereza na hata kujikuta ikipoteza tena kwa timu ya Bayern Munich kwenye Ligi Mabingwa.
Hali hiyo inaweza kuwapotezea hali ya kujiamini wakati ikija kukutana na Sunderland hasa pale ambapo Liverpool itakapokuwa imeshawazid kwa pointi.
Kwa sasa Liverpool haina mchezo ambao unailazimisha kusafiri umbali mrefu kama vile kwenda Ukraine au kusafiri kwenda safari ndefu kupambana na timu za Ligi na hivyo itakuwa haina kitu kinachowasumbua kuwafanya washindwe kuwa katika mazingira ya kombel hilo.
Sababu ya sita ni historia nzuri ya magoli ambapo hakuna mchezaji kwenye ligi kuu anaewafikia wachezaji kama vile Luis Suarez na Daniel Sturridge katika idadi ya magoli.
Kwa sasa wana magoli 38 ambapo Suarez anayo yake 23 huku Sturridge akiwa na 15 na hiyo ikiwa ni kabla ya mchezo wao dhidi ya Fulham.
Pia sababu ya saba ni uwezo wa mchezaji Steven Gerrard ambao umekuwa haukuwahi kuchukuliwa ni kama muhimu kwa kocha Sir Alex Ferguson (kocha wa zamani wa Manchester City) lakini amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake ya Liverpool.
Kutokana na uwezo wake huo akiutumia vema kwa kushirikiana na Suarez pamoja na Sturridge itakuwa ni fursa nzuri kwao kufanya mambo makubwa kwenye ligi hiyo na hatimae kuibuka na ushindi.
Sababu ya nane ni uwezo wa Mchezaji wa Liverpool, Raheem Sterling ambae anaendelea kukua kila kukicha na kuonesha uwezo mkubwa katika soka kuumiliki mpira na kusaidia upatikanaji wa magoli.
Hiyo inajidhihirisha katika mchezo safi aliouonesha kwenye mechi dhidi ya Arsenal, sasa mchezaji huyu akiwa anacheza kwa ukaribu zaidi na akina Suarez ni dhahiri kuwa ushindi ni lazima.
Kufuatia uwezo wake huo, umepelekea kocha wa timu hiyo Roy Hodgson kumchukuali mchezaji huo kama mrithi wa mchezjai Theo Walcott katika michuano ya Kombe la Dunia.
Mtandao huo umeonesha namna gani ambavyo Liverpool imejiimarisha katika kila idara, wachezaji hao wameweza kitumia vema mipira 22 iliyopotea kwa maana ya kutumia vema mipira iliyokuwa inakaribia kutoka.
Kwa uwezo wao huo wa kutumia mipira hiyo imezidi namna ambavyo Manchester City imefanya na imezidi kwa mara pia kwa Chelsea.