Wakazi wa Atlanta nao wamkataa Bieber
http://habari5.blogspot.com/2014/02/wakazi-wa-atlanta-nao-wamkataa-bieber.html
IWAPO msanii Justin Bieber akitimiza uamuzi wake wa kwenda jijini Atlanta kuishi sehemu wanayoishi wananchi wa kawaida huenda akakumbana na kadhia ya mgomo kutoka kwa kwa wananchi hao.
Wananchi hao wanaona kuwa uamuzi wake wa kwenda kuishi humo ni hatari kwa maisha ya watoto wao na jamii nzima kwa ujumla.
Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na chama cha malezi katika jimbo hilo katika mtandao wa kijamii wa Face book umesisitiza nia ya kuandamana kwa wananchi hao.
Watu hao hasa akinamama wameonekana kuwa na wasiwasi hasa katika suala zima la usalama wa watoto wao.
Walilalamika wakisisitiza kuwa amekuwa akituhumiwa kuendesha gari kwa spidi kali barabarani na amekuwa akifanya hivyo kwa muda na sasa haijulikana itakuwaje kwa hapo akiwa Atlanta.
Watu hao wamekuwa wakisisitiza kuwa ni vema msanii huyo akanunua eneo kubwa nje ya mji ambapo atakuwa na mambo yake huko.
Bieber amekuwa akilaumiwa kwa kuwa na matukio mbalimbali ya utovu wa nidhamu hasa kwa majirani zake.
Hivi karibuni alisababisha hasara ya mamilioni ya fedha kwa jirani yake mmoja huko Marekani baada yakurusha mayai katika nyumba yake anayoishi.