B Six kundi la muziki linalowashika Zanzibar
http://habari5.blogspot.com/2014/03/b-six-kundi-la-muziki-linalowashika.html
Kundi la kucheza muziki la B Six la kisiwani Zanzibar limewataka wasanii wa muziki wa kizazi kipya kisiwani humo kuwatumia katika video zao.
Kundi hilo ambalo limekuwa kivuti kikubwa katika uchezaji wa nyimbo za aina mbalimbali kuanzia Boliongo, muziki wa dansi na aina nyinginezo kwa sasa limekuwa likialikwa kwenye dhifa mbalimbali.
Akizungumza na safu hii mmoja kati ya wachezaji wa kundi hilo, afahamikae kwa jina la kisanii la Chipesti alisema kuwa kundi hilo linazidi kukua kwa sasa na linahitaji kusaidiwa.
Alisema kuwa ili kulisaidia kundi hilo ni vema wasanii wa nyimbo za kizazi kipya kuwatumia katika video zao pamoja hata shughuli nyingine.
Alisema kuwa kundi hilo linaweza kucheza kila aina ya nyimbo na kuongeza kuwa wanafanya shoo katika shughuli zote na hivyo kuomba kuungwa mkono zaidi.
Kundi hilo linaundwa na wasanii kama vile Sammar,Chipest,Kimange na Chawinde