Mfahamu Batalia msanii mshkaji wa karibu wa Chege
http://habari5.blogspot.com/2014/03/mfahamu-batalia-msanii-mshkaji-wa.html
MSANII Julio Batalia anaefanya kazi kwa ukaribu zaidi na msanii wa kundi la TMK Wanaume Family Chege Chigunda ameshaanza kutoa nyimbo akiwa na msanii huyo.
Batalia ambae aliwahi pia kushiriki katika shindano la Big Brother aliiambia safu hii kuwa akiwa na Chege kazi zake za muziki anaziona kuwa zinaenda poa zaidi.
Aliyaja baadhi ya nyimbo alizoimba na Chege pamoja na kundi la Mkubwa na Wanawe kuwa ni pamoja na Unanionaje alioimba na Mkubwa na Wanawe na wimbo mwengine ni Haina Noma alioimba na Chege na Madee.
Alisema kuwa pia kuna wimbo alioimba na Country Boy na mwengine ameimba na Jannette uitwayo You make me go.
"Kuna video mbili ambazo ule nilioimba na Country Boy pamoja na wimbo mwengine na Jannette ambapo kwa sasa nyimbo hizo zinafanya vema zaidi sokoni"alisema Batalia.
Aliongeza kuwa amejipanga kuimba na kupata fedha kupitia nyimbo zake na kuongeza kuwa yupo kamili kwa kazi za sanaa kwa kushirikiana na wasanii wengine.