Tukamwangalie Tunsiime
http://habari5.blogspot.com/2014/07/tukamwangalie-tunsiime.html
Na Evance Ng'ingo
MCHEKESHAJI wa Uganda anaejishughulisha na sanaa ya uchekeshaji wa majukwaani, Anne Kansiime atatoa burudani hapa nchini Agost 2 mwaka huu Golden Tulip, Dar es Salaam.
Anne ataungana na mchekeshaji mwengine kutoka Kenya Fredi Omondi pamoja na mchekeshaji aitwae Pilipili wa hapa nchini huku burudani ya muziki ikitolewa na bendi ya Odama.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na mratibu wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis ilifafanua kuwa kituo hicho kimemleta mchekeshaji huyo wa Uganda baada ya kutambua nafasi yake katika uchekeshaji.
“Kansiime ni mchekeshaji ambaye amejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa uwezo wake wa kuweka utani kwenye maisha ya kawaida’ alisema Francis.
Aliongeza kuwa" Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha".
Alisema kuwa mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Aliongeza kuwa burudani hiyo ya Kansiime, ambayo itakayoitwa Cheka Kwa Nguvu, itaanza saa moja usiku na kiingilio itakuwa tiketi zitauzwa shilingi elfu 90,000 kwa mtu mmoja, na shilingi 700,000 kwa meza ya watu nane.
======================