Basata yazifagilia tuzo za watu


Mdogo wake Steven Kanumba, Seth Bosco akichangia mawazo yake

Mhariri Mkuu wa Bongo 5 Media Group inayomiliki tovuti ya burudani ya Bongo 5 Fredrick Bundala akichangia

Mkurugenzi Mkuu wa Bongo 5 Media Group, Nancy Sumari akitoa mada kuhusiana na Tuzo za Watu

Kikao kikiendelea

Mshauri wa masuala ya Habari wa Tuzo za Watu Evance Ng'ingo akichangia kwa upande wake

Picha ya pamoja kati ya maofisa wa Basata na Bongo 5

Rama wa Bongo 5 akiwa kikaoni hapo

Kilifanyika nje ya ukumbi wa Basata

Wadau wa Basata wakichangia  
Habari  Kamili.
Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA, limeipongeza kampuni ya Bongo 5 Media Group kwa namna ambavyo imeendesha shindano la Tuzo za Watu zilizofanyika mwaka huu.

Katika kikao chake cha pamoja na kamati iliyoandaa tuzo hizo, Kamati inayoshughulikia ufuatiliaji wa masuala  ya Tuzo ya Basata iliyokuwa ikifuatilia tuzo hizo ilionesha kuridhishwa na namna ambayo imekuwa ikifanya kazi zake.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Malegesi alisema kuwa tofauti  na tuzo nyingine, Tuzo za watu zimeanza kwa muda mfupi lakini imejipatia umaarufu mkubwa kutokana na umakini wake katika uendeshwaji.

"Nawapongeza ingawaje kuna changamoto ndogondogo za hapa na pale lakini binasfi naona kuwa mmejitaidi na yale tuliyowakosoa myafanyie kazi kwa mwaka ujao"alisem Maregesi.

Kwa upande wake Nancy Sumari ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya uandaaji wa Tuzo za Watu alisema kuwa kamati yake imejipanga kuhakikisha kuwa kwa mwakani tuzo hizo zinaimarika zaidi.

Related

Sticky 6244038096427210637

Post a Comment

emo-but-icon

item