Usajili waongeezwa tena mbele mwisho leo
http://habari5.blogspot.com/2014/08/usajili-waongeezwa-tena-mbele-mwisho-leo.html
Na Mwandishi Wetu
DIRISHA la usajili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa wachezaji wazalendo limesogezwa mbele kwa Saa 48 zaidi tangia juzi na hivyo leo ndi mwisho.
Hatua hiyo ni kutokana na klabu nyingi kushindwa kukamilisha usajili katika muda uliotakiwa ambao ni juzi.
Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa alisema jana kuwa ni klabu ya JKT Ruvu peke yake ambayo imeshakamilisha usajili wake.
Alisema kuwa hali hiyo huenda ikawa imesababishwa na kushindwa kujua namna ya kutumia mfumo mpya wa elektroniki wa usajili.
Alisema kuwa kwa kutambua hilo TFF imeamua kusogeza mbele tena ili kuwapa muda ambapo muda huo ukiisha ndio inakuwa basi tena.
"Sisi kama waungwana tumeamua kuwasogezea tena muda mbele ili angalau na wao waweze kukamilisha sasa tangia jana (juzi) tumewaambia kuwa kesho (leo) ni ndio mwisho na watakaoshindwa ndo itakuwa basi tena"alisema Mwesigwa.
Aliongeza kuwa kwa timu za ligi daraja la kwanza ni timu moja tu ambayo ni Kimondo FC ndiyo ilifanikiwa kukamilisha usajili wake katika mfumo huo.
Aliwataka wahusika kukamilisha mapema kadiri wawezavyo huku akisisitiza kuwa dirisha la usajili kwa wachezaji wa kigeni litafungwa Septemba 6.
"Kwa dirisha la usajili kwa wachezaji wa kimataiga kama mnavyojua ni suala la kimataifa na lipo chini ya FIFA hivyo hatutakuwa na la kufanya kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa wanaendana na terehe hiyo iliyotajwa na kushindwa kufanya hivyo hakutakuwa na msaa zaidi"alisema Mwesigwa.
======================