CeeLo apatiwa ushauri nasaha
http://habari5.blogspot.com/2014/09/ceelo-apatiwa-ushauri-nasaha.html
MSANII wa muziki wa Marekani, CeeLo Green amejikuta akilazimika kupewa ushauri nasaha kutokana na ujumbe uliokutwa kwenye kurasa wake wa kijamii wa Twitter.
Aliandika ujumbe kuchangia mada kuhusiana na suala zima la ubakaji ambapo alijikuta akijichanganya.
Aliandika kuwa "iwapo kama nimejaribu kumbaka mtu na kisha nikashindwa kufanikiwa lakini mhusika akawa anataka inakuwaje"alihoji msanii huyo.
Kutokana na umaarufu wake muda mfupi baada ya kuandika ujumbe huo watu kadhaa walihamaki.
Wengi wao walianza mchakato wa kumshtaki kupitia vyama mbalimbali vya haki za binadamu.
Kampeni hiyo ilianza kwa kuitaka kampuni ya Warner Bross inayosimamia kazi zake kuachana na msanii huyo.
Ndani ya saa tatu tangia kuanza kwa kampeni hiyo saini zaidi ya 30,000 zilipatikana kuunga mkono hoja hiyo.
Wengi walikuwa wakimwelezea kuwa hata akiwa ni maarufu kwa kiasi gani kubaka sio suala la kuungwa mkono.
Hoja hiyo ilikuwa ni ngumu kwake na kujikuta akilazimika kuomba msamaha na kulazimika kuomba ushauri wa masuala ya kisaikolojia