Msikilize Miss East Africa 2012 kuhusiana na kilio chake cha zawada ya gari hadi leo

Huyu ndo mrembo wetu aliposhinda shindano hilo

Hakika ni mrembo hadi kawashinda hao wote

Pia ni Modo mzuri tena sana tu

Na Mwandishi Wetu
MSHINDI wa shindano la Miss East Afrika kwa mwaka 2012, Joselyn Maro amepeleka malalamiko yake kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) akilalamikia kutokabidhiwa nakala muhimu za zawadi yake ya gari alipowa kama mshindi.


Mrembo huyo alisema jana kuwa tangia apate ushindi wake huo alipewa gari aina ya Mazda ambalo hadi sasa hawezi kuliendesha kutokana na kutopewa kadi ya gari hilo.


Alisema kuwa hali hiyo kwake imekuwa ni ya wasiwasi kwa kuwa amelazimika kuliegesha gari hilo nyumbani akisubilia kukamilika kwa nakala hizo.


Alisema kuwa amekuwa akilazimika kuwasiliana na mratibu wa shindano hilo kampuni ya Lena Events bila ya mafanikio yoyote.


"Mimi nimekuwa nikimwomba kunisaidia suala hili la gari lakini ushirikiano umekuwa hakuna kabisa na niliamua kwenda Basata kuanzia mwezi Februali kuomba kusaidiwa na ndio ninasubiria majibu"alisema mrembo huyo.


Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Sanaa wa Basata, Vivia Sharua alikiri kupokea malalamiko ya Miss huyo na kusisitiza kuwa ofisi yake imekuwa ikifanya jitihada za kumpata mwandaaji huyo bila ya mafanikio.


"Sisi tumekuwa mara kwa mara tukimwandikia barua ya kumuita kwenye kikao lakini inaonekana kuwa amekuwa akituchenga"alisema Shalua.


Aliongeza" hilo gari linathamani ya Dola za Kimarekani 18,000 ambazo mmiliki wa gari hilo nae alikuja hapa Basata akilalamika kuwa hakupewa sehemu ya fedha za gari hilo kutoka kwa mwandaaji huyo na yeye anamdai huyo mwandaaji".


Aliendelea kufafanua kuwa kutokana na kutolipwa kwa fedha zake mmiliki alietoa gari hili alilazimika kuzuia kadi ya gari ili lisiweze kuruhusiwa kutumika.


Aliongeza kuwa baraza limeamua kumwandikia barua tena kwa mara ya mwisho mwandaaji huyo wa shindano hilo ikimwita katika kikao cha tathmini kitakachofanyika Septemba 24 mwaka huu katika ofisi za basata zilizopo Ilala.


Aliongeza kuwa kwa utaratibu mwandaaji wa shindano anatakiwa kukamilisha ripoti ndani ya mwezi mmoja tangia kumalizika kwa shindano lakini imekuwa tofauti kwa mwandaaji huyo ambapo kwa sasa ni takribani miaka miwili hajafika kwenye tathmini ya shindano lake.


"Kila akiitwa anakuwa na mambo yake mengine na hiyo imekuwa hivyo kuanzia mwaka 2012 sasa kwa sasa hivi Basata inae mwanasheria wake hivyo basi huo ndio mwisho wa huu ubabaishaji sisi tutalisimamia hadi huyo Miss apate haki yake"alisema Vivia.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Lena Events inayoandaa wa shindano hilo, Lena Calist alisema kuwa ofisi yake inaendelea kulishughulikia suala hilo.


"Kamati ya ufundi kwa sasa inaendelea na kulishughulikia suala hilo kwa na kila kitu kitakuwa sawa"alisema Calist.


Kuhusiana na kuitwa Basata alikiri kuandikiwa barua kipindi kilichopita na lakini hata hivyo alikuwa tayari kwenda kwenye kikao hicho kikaahirishwa.
============

Related

Sticky 2166404896530268911

Post a Comment

emo-but-icon

item