Diamond na Wema kushindania Tuzo Swahili Fashion
http://habari5.blogspot.com/2014/11/diamond-na-wema-kushindani-tuzo-swahili.html
Na Mwandishi Wetu
MWANAMUZIKI wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Nasib Abdul, Diamond Platinum anashindana na aliekuwa mpenzi wake Wema Sepetu katika kuwania Tuzo ya Mtu mwenye ushawishi mkubwa katika mitindo.
Tuzo hiyo zitatolewa kwenye Onesho la Mavazi la Swahili Fashion 2014 linaloandaliwa na Kampuni ya 361 Degrees na zitatolewa siku ya mwisho katika onesho la Swahili Fashion Week litakaloanza Desemba 5 hadi 7 mwaka huu
Katika shindano hilo wanaoshindana wengine ni pamoja na Mwamvita Makamba ambae namba yake ya kupigiwa kura ni SFW SY 01, Diamond Platnumz SFW SY 02, Millen Magesse SFW SY 03, Mohamed Dewji SFW SY 04 na Wema Sepetu SFW SY 05.
Pia Diamond anashindana katika kipengele cha wanaume wenye kuongoza huku namba yake ya ushiriki ikiwa ni SFW SMP 01 na anaochuana nao katika kipengele hicho ni pamoja na Luca Neghesti SFW SMP 01, Baraka Shelukindo SFW SMP 03, Noel Ndale SFW SMP, Rio Paul SFW SMP 05 na Juma Juxx SFW SMP 06
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa tuzo hizo, Haruna Ibrahim alisema kuwa kwa mwaka huu kuna ushindani mkubwa katika kila kipengele.
Aliongeza kuwa Meneja wa Msanii Wema Sepetu, Martin Kadinda nae anawania kipengele cha Mbunifu bora wa mchango katika tasnia hiyo ambapo anashindana na akina PSJ Couture SFW MWD 01,
Martin Kadinda. SFW MWD 02 Mtani Nyamakababi SFW MWD 03, Manju Msitta SFW MD 04 na Gabriel Mollel SFW MWD 05
Aliongeza kuwa pia kwenye kipengele cha mbunifu wa mavazi bora wa mwaka wanaoshindania Kadinda anashindana akiwa anaumana na akina Gabriel Mollel SFW ID 02, An Nisa Abayas SFW ID 03, Eve Collections SFW ID 04
Alisema kuwa kwa upande wa Baileys, mwanamitindo bora wa kike kwa mwaka huu wanaoshindana ni Jamilla Nyangassa ambae namba yake ya kupigiwa kura ni SFW FM 01, Gyver Meena SFW FM 02, Jihan Dimachk SFW FM 03, Neema Kilango SFW FM 04, Joceline Maro, SFW FM 05, Lethina Christopher SFW FM 06.
Kwa upande wa wanamitindo bora wa kiume wanaoshindania tuzo hizo ni pamoja na Danny David SFW MM 01, Victor Casmir SFW MM 02, Dietrich luhanga SFW MM 03, Ally Daxx SFW MM 04.
Haruna aliongeza kuwa kwa upande wa Tuzo za Mwanamitido bora wa mwaka kwa Afrika Mashariki wanaoshindaniwa ni pamoja na Vivian Mutesi (UGANDA) SFW EAM, Sharon Mirembe Sanya (UGANDA) SFW EAM 02, Christina Masese (KENYA) SFW EAM 03, Ajuma Nasenyana (KENYA) SFW EAM 04 Aliongeza kuwa kwa upande wa Tuzo ya Mbunifu wa mwaka wanaoshindania ni pamoja na Kiki's Fashion SFW DY 01, Jamilla Vera Swai SFW DY 02, Ailinda Sawe SFW DY 03,An Nisa Abayas SFW DY 04, Manju Msita SFW DY 05, Lucky Creations SFW DY 06
Pia aliongeza kuwa kutakuwa na tuzo ya mwaka kwa mtaalamu wa urembo na nywele na wanaoshindaniwa ni pamoja na Rehema Samo SFW HMA 01, Asila Makeup SFW HMA 02, Glambox SFW HMA 03, Lavie Makeup Studio SFW HMA 04
Pia wanaoshiriki katika kipengele cha kushindani tuzo ya vidani ni The Mabinti Center SFW AD 01, Enjipai Jewelleries SFW AD 02, Florinyah Designs SFW AD 03, Sairiamu SFW AD 04, Linda August SFW AD 05 na Nyumbani Designs SFW AD 06
Watakaoshindania tuzo katika kipengele cha mbunifu wa Afrika Mashariki wanaoshindania ni pamoja na Martha Jabo (Uganda) SFW EAD 0, Afrostreet Kollektions (Kenya) SFW EAD 02, Arapapa by Santa Anzo (Uganda) SFW EAD 03, Akinyi Odongo (Kenya) SFW EAD, Kiko Romeo (Kenya) SFW EAD 05 na Mille Colliness (Rwanda) SFW EAD 06.
Swahili Fashion Week na Tuzo za mwaka 2014 zinaandaliwa na 361 Degrees kwa usaidizi wa Hotel Sea Cliff, Sea Cliff Court, chini ya udhamini wa EATV, East Africa Radio, Baileys, Mercedes-Benz, 2M Media, Tanzania Printers LTD and Syscorp Media na Basata.