Usikose kufika katika usahili wa Swahili Fashion
http://habari5.blogspot.com/2014/11/usikose-kufika-katika-usahili-wa.html
Na Mwandishi Wetu
USAILI wa kutafuta wanamitindo watakaoshiriki katika onesho la Mavazi la Swahili Fashion Week 2014 unafanyika kesho (Jumamosi) katika Hoteli ya Sea Cliff.
Katika usaili huo vijana wa kiume na wa kike wanaombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki ili na watakaopatikana watashiriki kwenye onesho hilo litakalofanyika kuanzia Desemba 5 hadi 7 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mratibu wa usahili huo, Honest Arroyal alisema wanaoona kuwa wanavigezo vya kushiriki wajitokeze kwa wingi.
Alisema kuwa wanaangalia urefu, kujiamini pamoja na vigezoi vingine ambavyo mwanamitindo anatakiwa kuwa navyo.
Alisema kuwa kama inavyokuwa kwa miaka yote wale wenye vigezo ndio wanaochaguliwa kupata nafasi na aliwataka kwa mwaka huu kujitokeza wengi zaidi.
“Kupitia kuonesha mavazi katika shindano hili ndio ambapo wanamitindoi wanapata nafasi za kuonekana na kushiriki kwenye shughuli nyingine mbalimbali” alisema Arroyal.
Aliongeza kuwa wapo wanamitindo ambao wamepata kazi nje ya nchi kutokana na ushiriki wao kwenye maonesho kama hayo na kuongeza kuwa wengi wao wamefanikiwa.
Alisema kuwa Miss Universe hapa nchini mwahuu, Carolyne Bernard alishiriki Swahili Fashion mwaka jana na ndipo alipopatia uzoefu. Pia aliwataja wengine kuwa ni pamoja na Ali Dax ambae ni mwanamitindo wa kitanzania aliepo Afrika Kusini.
Katika onesho la Swahili Fashion mwaka huu wabunifu 24 kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki.
Swahili Fashion Week na Tuzo za mwaka 2014 zinaandaliwa na 361 Degrees kwa usaidizi wa Hotel Sea Cliff na Sea Cliff Apartments na kudhaminiwa na EATV,East Africa Radio,BASATA (Baraza La Sanaa La Taifa),2M Media, Baileys, Syscorp Media,Tanzania Printers Ltd,NexiaSJ, Fabcars na Eventlites.