2015 uwe wa mafanikio kwa wasanii
Na Evance Ng'ingo
ZIKIWA zimebakia siku tano kabla ya kuanza mwaka mpya wa 2015 ni vema wadau mbalimbali wa sekta ya sanaa wakajipanga kuufanya mwaka 2015 uwe mwaka wa mafanikio.
Hapa ninazungumzia kuanzia wasanii wenyewe wawe wanamuziki au waigizaji ambapo kwa pamoja kila mmoja ni  lazima hakikishe kuwa mwaka huo unakuwa ni wa mafanikio.
Mwaka huo unaweza kuwa mwaka wa mafanikio iwapo tu wahusika wakianza kuwa na mikakati mizuri ya kukuza kazi zao.
Mwaka huu unaomalizika ni mwaka ambao uwasukume kujitathmini kwa kuangalia ni nini walichokifanya na kuangalia kuona ni yapi wanatakiwa kuyafanya kwa mwaka huo ujao.
Mambo ya kujitathmini ni pamoja na kuangalia ni yapi ambayo hawakuyatimiza kwa mwaka huu na kisha kujipanga kwa mwaka ujao.
Kwa upande wa sanaa yapo mengie ambayo hata kwa msanii moja mmoja anaweza kuanza kuyapangilia kwa ajili ya mwakani.
Katika sanaa hasa ya muziki ni wakati kwa wasanii kuangalia kwa kiasi gani wanaweza kuimba au kuandika nyimbo zenye maana na ujumbe.
Kujipanga huko kunaweza kuwasaidia kufika mbali katika sanaa kama vile ambavyo amefanya msanii Nasib Abdul ambae mwaka 2014 umekuwa ni wa mafanikio kwa kuchukua tuzo katika shindano la Muziki la Chanel O, Afrika Kusini.
Kama alivyofanya msanii huyo basi ndio ambavyo hata wasanii wengine wanaweza kujipanga na kuhakikisha kuwa wanajituma na kufikia mafanikio kama hayo.
Mwisho wa siku tutajikuta Tanzania tunazidi kupaa juu katika sekta ya sanaa kwa kuwa tutakuwa na wasanii wengi wenye kutuwakilisha vema nje ya nchi.
Hii yote inawezekana kufanyika ila iwapo tu kukiwa na mikakati ambayo mara zote mwanzo wa mwaka ndio inafaa au inatakiwa kuwa na mikakati kama hiyo yenye tija.
Binafsi naona kuwa hata mshindi wa Tuzo za Big Brother mwaka huu Idris Sultan aliejishindia Milioni 524 nae ni mwaka wa kujipanga kuhakikisha kuwa anaanza 2015 kama mfano wa kuigwa.
Ninachotaka kusema hapa ni suala zima la umuhimu wa kujipanga kwa wadau wa sanaa kutumia vema mwaka ujao katika kuendeleza sanaa.
Kujipaga huko sio kwamba kunawahusu wasanii wa muziki tu peke yao, bali pia hata wadau wa sanaa kwa ujumla ambapo nawazungumzia hata waratibu wa Tuzo za Watu, Tuzo za Kili, Tuzo za Filamu na wengineo kwa ujumla kuwa wanatakiwa kujipanga mwaka 2015 kuzingatia zaidi suala zima la Umakini na Ubora wa kazi zao  za Tuzo.
Pia ni uwe mwaka wa kuhakikisha kuwa kazi za sanaa zisizokuwa na maadili mema katika jamii zinazuiwa kabisa kuingia mtaani.
Hiyo ni pamoja na Bodi ya Filamu nchini pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhakikisha kuwa kwa pamoja mwaka 2015 sekta hizo zinaangaliwa kwa jicho la tatu.
Aibu mbalimbali zilizojitokeza kwa mwaka huu mwakani hazijitokezi tena, kwa maana nyingine uwe ni mwaka wa kutoka maofisi na kwenda kusimamia sekta hizo za filamu na Muziki mitaani.

2015 uwe wa mafanikio kwa wasanii
Na Evance Ng'ingo

ZIKIWA zimebakia siku tano kabla ya kuanza mwaka mpya wa 2015 ni vema wadau mbalimbali wa sekta ya sanaa wakajipanga kuufanya mwaka 2015 uwe mwaka wa mafanikio.
Hapa ninazungumzia kuanzia wasanii wenyewe wawe wanamuziki au waigizaji ambapo kwa pamoja kila mmoja ni  lazima hakikishe kuwa mwaka huo unakuwa ni wa mafanikio.
Mwaka huo unaweza kuwa mwaka wa mafanikio iwapo tu wahusika wakianza kuwa na mikakati mizuri ya kukuza kazi zao.
Mwaka huu unaomalizika ni mwaka ambao uwasukume kujitathmini kwa kuangalia ni nini walichokifanya na kuangalia kuona ni yapi wanatakiwa kuyafanya kwa mwaka huo ujao.
Mambo ya kujitathmini ni pamoja na kuangalia ni yapi ambayo hawakuyatimiza kwa mwaka huu na kisha kujipanga kwa mwaka ujao.

Kwa upande wa sanaa yapo mengie ambayo hata kwa msanii moja mmoja anaweza kuanza kuyapangilia kwa ajili ya mwakani.

Katika sanaa hasa ya muziki ni wakati kwa wasanii kuangalia kwa kiasi gani wanaweza kuimba au kuandika nyimbo zenye maana na ujumbe.

Kujipanga huko kunaweza kuwasaidia kufika mbali katika sanaa kama vile ambavyo amefanya msanii Nasib Abdul ambae mwaka 2014 umekuwa ni wa mafanikio kwa kuchukua tuzo katika shindano la Muziki la Chanel O, Afrika Kusini.

Kama alivyofanya msanii huyo basi ndio ambavyo hata wasanii wengine wanaweza kujipanga na kuhakikisha kuwa wanajituma na kufikia mafanikio kama hayo.
Mwisho wa siku tutajikuta Tanzania tunazidi kupaa juu katika sekta ya sanaa kwa kuwa tutakuwa na wasanii wengi wenye kutuwakilisha vema nje ya nchi.
Hii yote inawezekana kufanyika ila iwapo tu kukiwa na mikakati ambayo mara zote mwanzo wa mwaka ndio inafaa au inatakiwa kuwa na mikakati kama hiyo yenye tija.

Binafsi naona kuwa hata mshindi wa Tuzo za Big Brother mwaka huu Idris Sultan aliejishindia Milioni 524 nae ni mwaka wa kujipanga kuhakikisha kuwa anaanza 2015 kama mfano wa kuigwa.
Ninachotaka kusema hapa ni suala zima la umuhimu wa kujipanga kwa wadau wa sanaa kutumia vema mwaka ujao katika kuendeleza sanaa.

Kujipaga huko sio kwamba kunawahusu wasanii wa muziki tu peke yao, bali pia hata wadau w
 sanaa kwa ujumla ambapo nawazungumzia hata waratibu wa Tuzo za Watu, Tuzo za Kili, Tuzo za Filamu na wengineo kwa ujumla kuwa wanatakiwa kujipanga mwaka 2015 kuzingatia zaidi suala zima la Umakini na Ubora wa kazi zao  za Tuzo.

Pia ni uwe mwaka wa kuhakikisha kuwa kazi za sanaa zisizokuwa na maadili mema katika jamii zinazuiwa kabisa kuingia mtaani.

Hiyo ni pamoja na Bodi ya Filamu nchini pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhakikisha kuwa kwa pamoja mwaka 2015 sekta hizo zinaangaliwa kwa jicho la tatu.
Aibu mbalimbali zilizojitokeza kwa mwaka huu mwakani hazijitokezi tena, kwa maana nyingine uwe ni mwaka wa kutoka maofisi na kwenda kusimamia sekta hizo za filamu na Muziki mitaani.

Related

Sticky 1023327401369315144

Post a Comment

emo-but-icon

item