Bieber ajinunulia ndege

MWANAMUZIKI Justine Bieber amenunua ndege mpya ikiwa ni zawadi yake ya sikukuu ya Christimass.

Mwanamuziki huyo ambae amekuwa akitamba zaidi mwaka huu na kuwa ni mmoja kati ya wanamuziki walijiingizia fedha nyingi kwa njia ya shoo, amefunga mwaka kwa kujinununulia zawadi hiyo ya aina yake.

Ndege hiyo ya aina yake ni kubwa na yenye kubeba watu 11 huku ikiwa na vitu mbalimbali vya kifahari.

Ni ndege ambayo ina nafasi kubwa ya kukaa watu ndani ikiwa pamoja na kuwa na viti vikubwa na vye kuvutia.

Akizungumzia gharama ya ndege hiyo alisema kuwa imegharimu Dola za Kimarekani Milioni 60 na amefurahia kutumia ahadi yake ya kujinunulia ndege.

"Kwangu kama msanii nimekuwa na nia ya kujipatia zawadi kubwa na yenye thamani zaidi kulingana na thamani yangu katika fani hii" alisema msanii huyo.
=============================

Related

Sticky 327800384415887917

Post a Comment

emo-but-icon

item