Tuungane na Fid Q katika hili

Na Evance Ng’ingo
MSANII wa Muziki Hip-hop Fareed Kubanda, Fid Q, amezindua kampeni maaluma ya kuhamasisha uzalendo kwa vijana wa kitanzania ijulikanayo kama Tuonane Januari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Fid Q alisema kuwa ameamua kuanzisha kampeni hiyo kwa lengo la kuwafikia wanajamii hasa vijana kuwataka kujihusisha kikamilifu katika masuala mbalimbali ya kimsingi.

Alisema kuwa vijana mbalimbali wamekosa mwamko katika kujihusisha na masuala mbalimbali ya vijana kama vile kupiga kura na kuendeleza harakati mbalimbali za kimaendeleo.

Aliongeza kuwa kwa kuona hali hiyo ameamua kushirikiana na wasanii wengine katika kufanya matamasha mbalimbali ya kuelemisha jamii ambapo ataanza na Njombe.

 “Kuna kitu kimoja ambacho watu wengi hasa hasa vijana wenzangu hawakifahamu, Nchi  yetu ni changa sana. Vijana nchi hii chini ya umri wa miaka 35 ni zaidi ya asilimia 80 ya idadi ya watu,

wakati watu wazima zaidi ya miaka 60 ni asilimia chini ya 5 ya watanzania wote. Hizi ni takwimu za sensa iliyopita na hivyoutaona nafasi ya vijana katika mambo mbalimbali hapa nchini”alisema Fid Q.

Aliwataka vijana kutambua pia nafasi zao katika kubadilisha jamii hasa kwa kutumia nguvu ya kura zao katika kuchagua viongozi bora hasa katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa unaoendelea, na uchaguzi mkuu wa 2015 ujao.

“lazima vijana tuamke na tushiriki kikamilifu, kwanza vijana wenye uwezo na sifa za kugombea nafasi za uongozi ni lazima wafanye hivyo, pili vijana wenye vigezo vya kupiga kura pia ni lazima wafanye hivyo maana ni wajibu wetu pia  vijana ni lazima tushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni ili kuhakikisha ishu zetu za msingi zinajadiliwa na wagombea na zinapewa kipaumbele.

Katika mkutano wake huo aliongozana na wasanii wengine mbalimbali ambapo kwa pamoja walionesha nia ya kusaidia vijana katika kusaidia jamii.
==============

Related

Sticky 6353281810925784733

Post a Comment

emo-but-icon

item