Tanzania kunufaika zaidi na umeme wa Solar

TANZANIA imeingia katika mpango wa kutumia Solar ujulikanao kama One Milion Solar Homes, wenye lengo la kuzipatia nyumba milioni moja huduma ya umeme wa uhakika na salama kufikia 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Lutengano Mwakahesya alisema kuwa mradi huo utasaidia ajira kwa vijana.

Alisema kuwa mradi huo utatoa umeme kwa silimia 10 ya watu nchini na pia kusiaida katikia upatikanaji wa ajira 15,000 zihusianazo na sola.

Alisema kuwa kwa sasa asilimia 86 ya watanzania wanategemea mafuta ya taa na mishuma kama njia kuu ya kujipatia mwanga hali ambayo haitoshelezi mahitaji husika.

Alisema kuwa kwa sasa mradi umeanza kufanya kazi kwa mikoa ya Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Mwanza na Geita ambapo gharama ya kujiunga ni shilingi 15,000 na mtumiaji anaweza kununua umeme kama manunuzi ya umeme wa kawaida.

"Yani mteja anaweza kununua umeme huo wa jua na kuingiza namba za kiasi alichonunua katika mita ya umeme wa jua na kisha kupata umeme hasa kwa watu wa vijijini ambapo mradi huu unafanya kazi, na lengo ni kuhakikisha kuwa nchi inaongoza katika mradi wa nishati ifikapo mwaka 2030"alisema Mwakahesya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Off Grid Electric, Erica Mackey alisema kuwa mradi huo ambao umekuwa na mafanikio makubwa katika nchi nyingi hasa zinazoendelea na kwa hapa nchini utakuwa ukijulikana kama M-Power Off Grid na malipo kwa siku ni shilingi 360.

Alisema kuwa kwa Tanzania imewekezwa zaidi ya bilioni 13 ambapo Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC) limetoa Bilioni tisa katika mradi wa kwanza wa kufikia nyumba zaidi ya laki moja.
============== 

Related

Technology 6953318036856436254

Post a Comment

emo-but-icon

item