Ali Kiba sahani moja na Diamond katika Tuzo za WatuT

WANAMUZIKI mahiri wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Nasib Abdul, Diamond, na Ali Kiba wanashindania Tuzo ya Msanii Bora wa kiume katika Tuzo za Watu 2015. Wasanii hao wawili kwa sasa ndio magwiji wa muziki huo hapa nchini huku kila mmoja akiwa na mashabiki wake na kila mmoja akiwa anajitamba kuwa ni ndio bora kwa sasa. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Bongo 5 Media Group inayoratibu Tuzo hizo, Nancy Sumari iliwataja wasanii wengine watano wanaowania kipengele hicho cha msanii bora pia. Wasanii hao ni pamoja na Elias Barnaba, Ommy Dimpoz pamoja na Jux. Katika kipengele cha wasanii msanii bora wa kike wanaowania ni pamoja na Lady Jaydee, Linah, Mwasiti, Shilole Vanesa Mdee. Pia Filamu ya Chausiku, Kigodoro, Madam, Mshale wa kifo pamoja na Sunshine zinashindana kwenye kipengele cha Filamu zinazopendwa. Msanii Jocob Steven, JB, na Raymond Kigosi, Ray, wanaumana pamoja katika kipengele cha mwongozaji bora wa filamu ambapo wengine nao wanaowania ni pamoja na Leah Mwendamsoke, Timothy Conrad, na William Mtitu. Katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike wa mwaka msanii Elizabeth Michael, Lulu, anaumana na Wema Sepetu, Irene Uwoya, Jacline Wolper pamoja na Riyama Ally. Jb pia anakuja kuumana tena na Mzee Majuto, Ray, Hemedi Suleiman pamoja na Salim Ahmed katika kipengele cha msanii bora wa kiume ambapo mwaka jana Jb aliumana na Mzee Majuto katika kipengele hicho na Majuto alishinda. Katika kipengele cha Video bora ya Video bora ya muziki video ya Akadumba ya Nay wa Mitego , KIpi Sijaskia ya Profesa Jay, Nani kama Mama ya Christina Bella, Wahalade ya Barnaba pamoja na XO ya Joh Makini. Kwa upande wa wanaoshindania kipengele cha Mtayarishaji bora wa Video za Muziki ni ABBY Kazi, Adam Juma, Khalfan, Hanscana pamoja na Nisher. Huku kipengele cha tovuti inayopendwa zaidi zinazoshindaniwa ni pamoja na dj choka, Jamii Forum, Michuzi, Millardayo, Timesfm. Kipindi cha Luninga kinachopendwa ni pamoja na Friday Night Live, In My Shoes, Mkasi, Planet Bongo na Take One, huku mtangazaji anaependwa wanaoshindana ni Salama Jabir, Salim Kikeke, Sam Misago, Zamaradi Mketema na Dullah Ambua. Kipindi cha Radio kinachopendwa ni Ala za Roho, Amplifaya, Hatua Tatu, Papaso XXL na Mtangazaji anaependwa ni Dida, Diva, D’ Jaro, Mariam Kitosi na Millar Ayo. Akizungumzia namna ya upigaji wa kura kuwachagua washindi Nancy alisema kuwa wananchi wanatakiwa kufuatilia katika mitandao ya kijamii pamoja na kusikiliza radio na kuongeza kuwa Tuzo hizo zinalenga kuwawezesha watanzania kuwa karibu zaidi na watu wao wanawapenda kwa kuwachagua.

Related

Sticky 271336048807964889

Post a Comment

emo-but-icon

item