Ifahamu Party ya Zall All White ilivyokuwa

Na Evance Ng'ingo MAELFU ya watanzania walijitokeza juzi kwenye Sherehe ya Zari White Party iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo wasanii na wengineo. Sherehe hiyo imeandaliwa na mwanadada Zari Hassan mganda aishie hapa nchini ambae ni mpenzi wa mwanamuziki mahiri wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul,Diamond. Hafla hiyo iliyoanza saa moja ilihusisha zaidi vazi jeupe ambapo asilimia 95 ya waliohudhuria walikuwa wamevalia mavazi meupe huku ikipambwa na burudani safi kutoka kwa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva. Nje ya ukumbi huo kabla ya kuingia kwenye ukumbi mkubwa kulikuwa na jukwaa ambalo wasanii wa Bongo Fleva kama vile Makomandoo na wengineo waliimba na kucheza. Hiyo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuwaburudisha wageni kabla ya kuanza kwa sherehe kamili na ilipotimu saa mbili mlango mkubwa ukafunguliwa na wageni wakaanza kuingia ndani. Humo ndani kulikuwa na jukwaa moja kubwa na sehemu tatu tofauti zimetengwa ambapo kulikuwa na sehemu ya watu waliolipa Milioni tatu, waliolipa milioni moja na waliolipa lakini moja huku wale wa elfu 50. Wachezeshaji mbalimbali wa muziki (DJ) walikuwa wakichezesha muziki humo ndani kabla ya kuwasili kwa wapenzi hao Zari na Diamond ambapo kwa sasa ni moja kati ya wapenzi wanaozungumzwa zaidi kwa Afrika Mashariki wakijulikana zaidi kwa jina la Zarimond. Ilipofika majira ya saa nne waliingia ukumbini hapo huku wakiwa wamesongwa na mashabiki wao wakiimba nyimbo za Diamond huku wengi wakitaka kupiga nao picha katika Red Carpet. Huku muda huo ndani kulikuwa na burudani kutoka kwa wasanii kama vile Weusi pamoja na Ruby, wakati Ruby akiwa anaendelea kuimba ndipo Zari na Diamond wakaingia na muda huo watu wakawageukia na kuanza kuwashabikia huku wakizidi kuwasonga. Baada ya dakika 10 Diamond alialikwa jukwaani ambapo nae alikuwa amevalia suti nyeupe na aliwashukuru watu waliohudhuria na kisha kumkaribisha Zari jukwaani. Alipotaja jina la Zari watu walishangilia kwa sauti kubwa huku wakiliita jina lake na hata mwadada huyo alipopanda aliishia kwanza kulia kwa furaha na alisema kuwa haamini namna ambavyo watanzania wamempokea. "Ninafurahi kuwa Tanzania na mnajua kuwa ninawazalia mtoto wenu yani mtoto mtanzania kwa hiyo nini ni sawa na mtanzania mwenzenu nashukuru mlivyonipokea na ninawapenda sana nyie ni watu Wema" alisema Zari. Alipoondoka ziliendelea burudani kadhaa jukwaani hapo na ilipofika zamu ya Diamond aliimba nyimbo zake zote huku akishangiliwa na mashabiki hao hasa alipokuwa akilitaja jina la Zari kwenye nyimbo ambazo awali alitaja jina la Wema au wasichana wengine aliokuwa na uhusiano nao. "Najua kwa sasa Zari ni mama mtarajiwa wa mtoto wangu na si mnajua tena ndo shemeji yenu na ndo wifi yenu sasa hapa ni sherehe yake ni kama tunamkaribisha fulani" alisema Diamond. Burudani ilinoga zaidi hasa pale alipoanza kuimba na Ney wa Mitego wimbo wao uitwao Muziki gani, kwa kuwa muziki huo unahusisha vijembe na hasa pale ambapo Ney wa Mitego anamsema Diamond kuwa anawachezea wanawake na ndipo likatajwa jina la Zari tena. Waliendelea na vijembu huku muziki umezimwa na hapo ilikuwa imefika saa nane usiku na huku watu wakiwa ni kama ndio sherehe imeanza burudani ilikuwa safi na asilimia kubwa ya waliohudhuria walifurahishwa na burudani hiyo. ==============

Related

Technology 6423338752642466860

Post a Comment

emo-but-icon

item