Jide amshirikisha Uhuru katika ngoma hii

MWANAMUZIKI wa muziki Bongo Fleva, Judith Wambura, Lady Jaydee ameachia wimbo wake mpya akimshirikisha mwanamuziki Uhuru wa Afrika Kusini.

Wimbo huo unaitwa Give Me Love ambao una maadhi ya blues huku ujumbe wake mkubwa ukiwa unahusiana na masuala ya mapenzi.

Akizungumzia wimbo huo, Lady Jaydee alisema kuwa ni wimbo ambao unalenga kumtangaza zaidi katika anga la muziki bara Afrika hasa akiwa kama mwanamuziki kutoka Afrika Mashariki.

Alisema kuwa ametumia muda mwingi kuanzia kuuandaa wimbo huo hadi kufikia hatua ya kurekodi na kuuimba.


"Mimi bado ninaendelea na harakati zangu za kulitafuta soko la dunia kwa kuwa ninaamini kuwa nina kipaji kikubwa cha kuweza kufanya hivyo na kwa hiyo nimeamua kuanza kwa kuimba na Uhuru mwanamuziki ambae anafahamika kwa uwezo wake"alisema Lady Jaydee.

Aliongeza kuwa " Huu ni wimbo ambao ninamini kuwa utafanya vema katika soko la muziki hapa nchini kwa kuwa umeandaliwa vema kuanzia kuimbwa hadi kurekodi kwake".

Kuhusiana na suala zima la Video ya wimbo huo, Lady Jaydee alisema kuwa inatarajiwa kuingia sokoni mwezi ujao kwa kuwa kwa sasa bado haijakamilika.

Alisema kuwa inaandaliwa nchini Afrika Kusini na inatarajiwa kuwa video yenye hadhi ya kimataifa.

Ni wimbo ulioandaliwa na mtayarishaji mahiri wa muziki nchini Afrika Kusini Dj Maphorisa.

Lady Jayde ni moja kati ya wanamuziki wakongwe hapa nchini ambao wamechangia maendeleo ya muziki wa Bongo Fleva huku kwa sasa akiwa anamiliki bendi yake pa moja na mgahawa wa chakula na kipindi cha Luninga.
===================

Related

Technology 4095583937565185895

Post a Comment

emo-but-icon

item