BOA banki yajumuika na wagonjwa wa CCBRT
http://habari5.blogspot.com/2015/04/boa-banki-yajumuika-na-wagonjwa-wa-ccbrt.html
Wasanii wa kundi la Claudia wakicheza na wagonjwa waliolazwa kwenye hopsitali ya CCBRT wakati walipoenda hospitalini hapo kuburudisha, hafla hiyo iliandaliwa na Benki ya Afrika, Boa |
Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Benki of Afrika, BOA, Wasia
Mushi akiwahudumia chakula watoto waliolazwa kwenye
hospitali ya CCBRT ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka na watoto
hao
Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Benki of Afrika, BOA, Wasia
Mushi akikabidhi misaada ya aina mbalimbali kwa watoto waliolazwa kwenye
hospitali ya CCBRT ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka na watoto
hao
habari kamili.
Na Mwandishi Wetu, Evance
JAMII imetakiwa kuendelea na moyo wa kuwasaidia wagonjwa wa
aina mbalimbali hasa watoto hususan kwenye kipindi cha sikukuu kama vile Pasaka
na nyinginezo.
Wito huo ulitolewa juzi na Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa
Benki of Afrika, BOA, Wasia Mushi wakati akizungumza na waandishi wa habari
katika Hospitali ya CCBRT ambapo wafanyakazi wa benki hiyo walioenda
kusherehekea sikukuu ya Pasaka na wagonjwa.
Alisema kuwa wagonjwa wanahitajia faraja kutoka kwa watu
mbalimbali na wao wakiwa kama wafanyakazi wa benki wameona kuwa ni vema
wakatumia sikukukuu hiyo kusherehekea na wagonjwa hao.
"Hii ni sikukuu kubwa tena sana lakini wakati watu tukiwa
majumbani mwetu na watoto wetu tutambue kuwa wapo watoto na watu wengine
wamelazwa na hawana nafasi ya kushiriki sherehe kama hizi" alisema Mushi.
Mushi alisema kuwa pia imekuwa ni wasaha mzuri kwa wafanyakazi
wa benki hiyo kuungana na wazazi wa watoto hao ambao wanawauguza hospitalini
hapo.
Wakiwa hospitalini hapo wafanyakazi hao wa benki waligawa
zawadi mbalimbali kwa wagonjwa pamoja na kula nao chakula cha mchana.
Pia walitoa zawadi za vifaa vya kusomea kama madaftari, kalamu
pamoja na mifuko ya kubebea vifaa hivyo.
Watoto pamoja na wazazi wao walipata nafasi ya kucheza michezo
mbalimbali wakishirikiana na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mama mzazi wa mtoto Joseph Mali, Maria, alisema kuwa kwa
upande wake na mtoto wake wamefurahishwa na misaada hiyo na imekuwa ni faraja
kubwa kwao.
"Tumecheza muziki tumefurahia na kujiona kuwa tupo pamoja
na wenzetu yani hata mwanangu amefurahi na kujikuta akila na kushiba
kabisa". alisema Maria.
=========