Lil Wayne atangaza kuuza nyumba




California Marekani

MWANAMUZIKI wa Marekani, Lil Wayne ametangaza kuuza jumba lake la kifahari lililopo kwenye fukwe ya Miami.

Jumba hilo linauzwa kwa kitita cha Dola za Kimarekani Milioni 18, huku likiwa lina Vyumba tisa vikubwa vya kulala, mababafu makubwa pamoja na bwawa la kuogelea.

Lipo karibia na fukwe ya bahari huku likiwa ni kubwa na linavutia hasa kwa watu maarufu kuishi.

Lakini licha ya kutanagza kuuza jumba hilo limekuwa likizungukwa na maaskari hasa kutokana na kuhisiwa kuwa kuna uwezekano wa kuwapo kwa matukio ya kiharifu.

Lakini pia wakati huo huo mwanamuziki huyo amesema kuwa anataka kumchukulia hatua za kinidhamu mtu aliyempiga mlinzi wake.

Mlinzi wa mwanamuziki huyo alipigwa ngumi akiwa katika klabu ya usiku na mtu asiejulikana lakini mwanamuziki huyo alisema kuwa atahakikisha kuwa anampata na kumchukulia hatua za kinidhamu.

================

Related

Sticky 3078523709044042206

Post a Comment

emo-but-icon

item