Mfahamu Aika Lawere na harakati zake za kumuinua mwanamke



Na Evance Ng'ingo
WANAWAKE wengi hapo nchini wamekuwa wakihamasishwa kujiuma na katika kutafuta maisha hasa kwa kujihusisha na masuala mbalimbali ya biashara na mengineo.
Wapo wanawake ambao wameitikia vema wito huo na kuanzisha biashara za aina mbalimbali ambazo zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuendesha maisha yao.
Licha ya juhudi zao hizo katika kujituma kwenye kutafuta kipato lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kitaaluma hasa kwenye kuendesha biashara zao hizo ambapo wanahitaji msaada wa kitaaluma utakaowawezesha kuendesha biashara zao.
Haika Lawere ni mmoja kati ya wanawake ambao wameamua kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wenzao kukabiliana na changamoto hiyo.
huyu amekuwa akishiriki kwenye mijadala mbalimbali yenye lengo la kuwaelimisha wanawake wenzake kuhusiana na njia bora za kufanya biashara zao.
Haika ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake Biashara kwa Wajasiriamali Wanawake Tanzania (Tibwe) ambao umejikita katika kuwaelimisha wanawake masuala ya biashara.
Pia ni Mmiliki wa hoteli ya Mbezi Garden iliyopo Mbezi, Dar es salaam.Haika ambe ni msomi mwenye Shahada ya Uzamili katika masuala ya Utawala na Teknolojia ya Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Salford kilichopo jijini Manchester Uingereza.Baada ya kumaliza masomo yake hayo mwaka 2005 alirejea nyumbani na kuamua kuendesha biashara hiyo ya Mbezi Garden ambayo ni biashara ya familia.
Anasema kuwa tangia akiwa kwenye miaka ya 20 alikuwa akivutiwa na wanawake ambao wamepata mafanikio hasa wale waliokuwa na umri mdogo.
Anasema kuwa hiyo ilikuwa ni moja kati ya vitu ambavyo vilimfanya asome kwa bidii akiwa anajua kuwa ipo siku atakuwa na kitu cha kumwezesha kusimama na kuzungumza na wanawake wenzake.
Anaongeza kuwa alipohitimu masomo yake na kurejea nyumbani aliamua kujikitia zaidi katika biashara ya Hoteli hiyo ya Mbezi Garden hasa katika kuiendesha kibiashara zaidi na kuipa hadhi ya kisasa.
Anaongeza kuwa baada ya kuanza kuiendesha na kuongeza wigo mkubwa zaidi wa utoaji wa huduma zake aligeuza jicho kwa wanawake wenzake na kuona ni kwa kiasi gani anaweza kuwasaidia.
"Najua hiyo ipo kwenye maisha yangu miaka mingi yani kuona ni kwa kiasi gani ninashiriki kwa ukaribu zaidi katika kuwainua wengine hasa wanawake wale ambao wamejikita katika biashara" anasema Aika.
Anaongeza kuwa "nilipohakikisha kuwa huduma ya hoteli imesimama na kuwa tena ya faida na huduma nzuri zaidi nikaanza huduma ya ushauri wa kibiashara kwa wanawake wenzangu ili nao wafikie mbali zaidi".Anaendelea kufafanua zaidi kuwa ameongeza nyumba, kumbi ya harusi huku akiwa anatoa huduma za harusi, chakula mapambo na vinywaji katika hoteli yake hiyo.

Ubunifu ni moja kati ya mambo ambayo anatilia mkazo zaidi hasa akiwa anawafundisha wanawake wenzake kuhusiana na  biashara.

Anasema kuwa kuna siri kubwa ya mafanikio imejificha ndani ya suala zima la ubunifu ambapo wanawake wengi wameshindwa kulitambua.Anasema kuwa ubunifu ndio unaoweza kumwinua mwanamke na kumfanya kuwa mwenye mafanikio makubwa zaidi katika biashara ya aina yoyote ile.
Anaongeza kuwa kwa kuwa ubunifu ni hali ya kuongeza ufanisi katika kitu na kukifanya kuwa chenye upekee zaidi.Hivyo hasa kama mwanamke akiwa anafanya biashara ya kuuza keki anatakiwa kutambua kuwa wapo wanawake wenzake wengi ambao nao pia wanafanya biashara ya aina hiyo hiyo.
Ili kwa mwanamke kuwa wa kipekee katika huduma yake na asifanane na wengine anatakiwa kuhakikisha kuwa anakuja na wazo la kiubunifu ambalo linaweza kumwinua zaidi.
Anaongeza kuwa keki zinaweza kuwa zoteni bora na tamu lakini kuna anaweza kutokea muuzaji mmoja akatumia ubunifu wa kujitangaza zaidi na akawa amewaacha wenzake wote."Ubunifu unagusa zaidi katika suala zima la namna ya kuwa na kazi yenye ubora zaidi ikiwa ni pamoja na kujitangaza kibiashara zaidi kwa lengo la kuwashika wateja pamoja na mambo mengine yenye kulenga kuleta tija katika biashara"Anasema kuwa amekuwa akiwafundisha wanawake masuala hayo kwa muda mrefu sasa ambapo ni miaka minne tangia aanze kazi yake hiyo.
Anaongeza kuwa anaona kuwa kila kukicha kuna maendeleo katika kampeni nzima ya kuwataka wanawake kujiajili na kuwa wajasiriamali.
Anasema kuwa katika mafunzo ambayo amekuwa akiyafanya amekuja kugundua kuwa wapo wanawake wengi ambao wamebuni biashara endelevu na zenye kuweza kuleta maendeleo makubwa.
Anaongeza kuwa wapo wanawake ambao kwa sasa wanamiliki makampuni makubwa ya biashara ili hali walianza kama wajasiriamali wa kawaida tu.
Anaendelea kufafanua kuwa hiyo yote inatokana na hamasa ambazo watu mbalimbali wamekuwa wakitoa kwa wanawake kwa njia ya semina na makongamano mbalimbali.
Haika ameshiriki pia katika makongamano mbalimbali ya kibiashara kwa wanawake kuanzia ya ndani na nje ya nchi.
Alikuwa mjumbe katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya Ushirikiano kati ya China na Tanzania ambapo kulikuwa na wanawake wengi ambao walihudhuria na alikuwa na nafasi ya kuzungumzia masuala ya wanawake na ujasiliamali.
Pia aliwahi kualikwa kwenye mjadala uhusianao na Uwezeshwaji wa Biashara kwa Wanawake Wajasiriliamali wa Marekani ambapo alibadilishana nao uzoefu wa utendaji wa biashara kwa wanawake wa Tanzania na wa huko ambapo aligusia zaidi suala zima la faida ya ushirikiano wa kibiashara.
Alitangaza aina ya biashara kutoka kwa wajasiriamali wa Tanzania na kutafuta soko kwa wale wa Marekani.Mwanadada huyo mwenye ushawishi katika kundi la wanawake wenzake hasa wale wanaojihusisha  na masuala uelimishaji wa mambo ya biashara.
Ni mama wa watoto watatu ambao ni Paxton (8), Haris(7) na Princes (5) ambapo anasema kuwa watoto wake hao hawaathiri harakati zake katika kusaidia jamii."Mimi ni mama mwenye furaha na familia yangu ya watoto watatu na mume wangu kwa pamoja wananiongezea amani kwa kuwa ninakuwa na muda wa kutosha wa kuwa na familia yangu pamoja na ule wa kuwa na shughuli zangu za kikazi kama kawaida"anasema Haika.Anaongeza kuwa "ninafauraha pia kwa kuwa hawa watoto wangu wamekuwa wakifanya vema sana darasani na namshukuru Mungu kwa hilo sababu ninajiona ni kama sio mwenye kazi kubwa ya kuwasihi kusoma kwani wanapenda kufanya hivyo wenyewe na ndio maana wanaongoza".
Anaongeza kuwa katika maisha yake ya kawaida anapenda kusoma vitabu, kusikiliza na kucheza muziki pamoja na kuwa karibu na watu wapya na kukaribisha mawazo mapya.
Anaongeza kuwa akiwa kama mwanadada mjasiriamali pia anapenda kuona kila kile anachokifanya kuhusiana na biashara zake kinakuwa na mafanikio.
Anapenda kuwa karibu na wale wenye mafanikio ili kujifunza kutoka kwao na pia anapenda zaidi kuanzisha vitu vipya.Kwa kifupi huyu ni mwanadada ambae hapendi kubweteka na kukubali kuiona hata dakika moja kutoka kwake ikipotea hivihivi bila ya yeye kuwa na kitu cha kuingiza iwe mawazo mapya au fedha.
Mchaga huyu ameamua kuongeza wigo zaidi wa biashara kwa kuchukua zabuni ya kuongoza hoteli ya Nelly's Inn iliyopo Mbezi Africana, hapo anajihusisha zaidi na suala zila la uendeshaji wa hoteli hiyo.
Anaongeza kuwa kwake hakuna kitu kinachoitwa changamoto kwa kuwa kila anapokutana nazo huwa anaziona ni kama fursa zinakuja kwa namna tofautii.
"Mimi ni mmoja kati ya watu ambao yani hatuamini kabisa suala zima la kushindwa kwa kuwa kuna kila njia za kukabiliana na kushindwa huko ambazo zinatakiwa kwanza kama mjasiriamali kuzijua na kisha kujipanga kukabiliana nazo"anasema Haika.Anasema kuwa kwa upande wake kwanza kabisa huwa anahakikisha kuwa anashirikisha kila wale ambao anaona kuwa wanaweza kumsaidia kwa kila hali hadi anahakikisha kuwa anafanikiwa.Mwanadada Sonia Mataro ambae anajihusisha na utengenezaji wa keki anasema kuwa kwa upande wake amenufaika na elimu ya ujasiriamali inayotolewa na Aika kwa kuwa imempatia mwanga zaidi wa kutambua mianya ya biashara zake.Anaongeza mafunzo yanamsaidia kujua thamani zaidi ya kazi zake pamoja na kujua ni kwa kiasi gani kuna safari inayomngojea katika mafanikio.Mwanadada Jeniffer Shigholi ambae anasema kuwa amepata mafanikio kwenye biashara zake kutokana na msaada mkubwa wa kimawazo kutoka kwa Aika hasa akiwa kama mshauri wake na mwongozaji mkubwa wa biashara zake.==




Related

Technology 4372082758921040251

Post a Comment

emo-but-icon

item