ZFH yaja na shoo kali ya mavazi Zanzibar

Mmiliki wa Kampuni ya Black Fox Modeling Atu Mynah akizungumza na wanamitindo waliojitokeza kwenye usaili wa onesho la Divas Night litakalofanyika Zanzibar Ijumaa
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Zanzibar Fashion House, Farhiya Mayow, maarufu kama Titi akizungumza na wanamitindo hao

Mbunifu wa mavazi ambae pia ni mwanamuziki, Annette Ngongi wa lebo la Seghito akizungumza na wanamitindo hao,
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Zanzibar Fashion House (ZFH) inayoandaa onesho la mavazi la Diva's Night imechukua wanamitindo watano kutoka kampuni ya Black Fox Modeling kwa ajili ya onesho la Ijumaa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Afisa Mtendaji Mkuu wa ZFH, Farhiya Mayow alisema kuwa onesho hilo la aina yake litafanyika Kendwa Rock, Zanzibar.

Alisema kuwa onesho hilo linalenga kuitangaza Zanzibar na kuonesha uzuri wa vitu mbalimbali unaopatikana kisiwani humo huku akiwataka wadau zaidi kujitokeza kudhamini.

Alisema kuwa muda umefika kwa watu kuendeleza fani ya mitindo na kuongeza ajira kwa wananchi kupitia fani hiyo.
Alisema kuwa mwanamitindo Annette Ngongi ni moja kati ya wanamitindo ambao wataonesha mavazi siku hiyo na aliwataka wakazi kujitokeza kwa wingi.

" Najua Zanzibar inajulikana na kufahamika zaidi katika masuala ya utalii na hasa ule wa kihistoria lakini kuna pia masuala ya utalii wa utamaduni na mengineo hivyo basi onesho hili la Mavazi linalenga kabisa kuendelea utamaduni wa mavazi kwa kisiwani Zanzibar" alisema Farhiya.

Kwa upande wake Atu Mynah ambae ni Mkurugenzi wa Black Fox Modeling Agency alisema kuwa kampuni yake inatambua nafasi ya onesho la mavazi katika kuwaendeleza vijana.

Aliwataja wanamitindo waliojipatia nafasi ya kushiriki katika onesho hilo ni pamoja na Dinah David, Jessy Richard, Glory Gideon, Melody Miranda pamoja na Jean Butanga.

" Kampuni hii imekuwa ikiwaelimisha vijana wengi katika fani ya mitindo hasa kwa kuwaeleza kuhusiana na faida na njia mbalimbali za kufanya kazi  hii, na kwa sasa kushiriki katika onesho hilo ni hatua moja muhimu katika kuwaendeleza wanamitindo kupitia fani yetu hii" alisema Atu.

Kwa upande wake mmoja kati ya wanamitindo watakaoonesha shoo siku hiyo, Annette Ngongi wa lebo ya Seghito aliwataka watanzania kuendelea kuipenda fani ya mitindo hasa kwa kuvaa nguo zilizobuniwa na wabunifu wa ndani.
=========================

Related

Sticky 427662544422261623

Post a Comment

emo-but-icon

item