Mambo yazidi kunoga BSS

Na Mwanahabari Wetu
SHINDANO la Bongo Star Search, BSS, linazidi kuchanja mbuga ambapo kwa sasa washiriki wengine wawili jana waliyaaga mashindano hayo.

BSS shindano linaloandaliwa na kampuni ya Benchmark Production kwa mwaka huu limefikia mwaka wake wa nane na limedhaminiwa na Salama Condom, kinywaji cha Coca Cola pamoja na kampuni ya ndege ya Fast Jet.

Washiriki hao wameaga shindano hilo huku likiwa limeshaingia katika hatua ya kumi bora ambapo ni ya washiriki wengi kujifua zaidi katika kuhakikisha kuwa wanaingia kwenye kipengele cha ushindi.

Walioaga shindano hilo ni pamoja na Furaha Charles kutokea mkoani Mbeya pamoja na Emmy Wimbo ambae yeye ametokea hapa hapa Dar es salaam.

Washiriki hao walitolewa kwa kuwa kura zao hazikutosha lakini walionesha uwezo mkubwa wa kuimba hasa kutokana na mafunzo waliyopewa na walimu wa shindano hilo.

Kwa upande wake Furaha akizungumzia kuhusiana na shindano hilo alisema kuwa ni shindano ambalo limemfundisha mengi zaidi hasa kujua namna mbalimbali za uimbaji na uchezaji.

Pia Wimbo kwa upande wake alisema kuwa mbali na kutolewa kwenye shindano hilo lakini amejengewa msingi mzuri wa kuimba ambao anaahidi kuwa atatumia katika kujiendeleza zaidi.

Jaji Mkuu wa BSS, Ritha Paulsen akiungumzia kwa hatua iliyofikia shindano hilo kwa sasa alisema kuwa mambo yanazidi kupamba moto na kuwataka wananchi kuwapigia kura washiriki wanaowata kuendelea kuwapo kwenye shindano hilo.
====

Related

Sticky 3645668808987872234

Post a Comment

emo-but-icon

item