Flaviana Matata: Mwanamitindo, Mjasiriamali Mwanaharakati

Mwanamitindo Flaviana akiwa na Mbunifu wa Mavazi Mgese Mkory ambae ndio alibuni gauni la siku hiyo la Flaviana

Flaviana akiwa na rangi zake za kucha
MWANAMITINDO Flaviana Matata sio jina geni masikioni mwa watanzania na wadau wengine mbalimbali wa masuala ya mitindo duniani.

Alitokea katika shindano la Miss Universe na kuanzia hapo alianza safari ya kuwakilisha ngazi za kimataifa zaidi katika tasnia ya mitindo.


Makazi yake kwa sasa ni nchini Marekani na amekuwa akishiriki katika maonesho kadhaa ya kimataifa ya mitindo pamoja na matangazo ya biashara ya bidhaa za kimataifa.


Amekuwa akipamba majarida mbalimbali makubwa ya mitindo duniani huku sura yake ikitumiwa pia katika kuhamasisha maendeleo katika kampeni mbalimbali kubwa.
 

Flaviana na misaada ya elimu nchini
Kwa hapa nchini kwa siku za hivi karibuni amekuwa akijikita zaidi katika masuala mbalimbali ya kijamii hasa kusaidia sekta ya elimu.


Flaviana ameonesha nia thabiti ya kusaidia kutatua changamoto za elimu kwa hapa nchini kwa kuwa na staili yake katika kufanikisha adhma yake hiyo.


Mwanamitindo huyu amekuwa akitumia zaidi jina lake katika kutafuta misaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo na kutumia kuwasaidia wanafunzi.


Amewaingia wanafunzi kwa kutumia staili ya kusaidia mabegi, madaftari pamoja na kalamu ambavyo vyote hivyo vimewekwa jina lake.


Kwa njia hiyo wanafunzi zaidi ya 40000  wamenufaika na msaada huo kutoka kwa mwanamitindo Flaviana huku akiwa anawasomesha wanafunzi 20.


Wanafunzi hao zaidi ya 40000 amekuwa akiwasaidia kwa njia mbalimbali kama vile misaada ya madaftari, kalamu na mabegi ya shule.


Hadi sasa ameshafikia mikoa ya kanda ya Ziwa na kuwasaidia wanafunzi kadhaa wa shule za msingi na pia katika mkoa wa Lindi ameufikia kutokana na ufadhili kutoka kwa wahisani mbalimbali.


"Mimi kwa miaka mingi nimekuwa nikiguswa na suala zima la kusaidia wanafunzi na hasa zaidi kwa kuwaingia kwa kuwasaidia kile kitu ambacho kinawagusa moja kwa moja"anasema Flavina.


Alisema " ninapenda kuwafikishia kile ambacho wao wanajitaji kuna mahala wanakuwa wanahitaji ujenzi wa vyoo basi au wengine madaftari au kalamu sasa ninawafikishia huduma kulingana na uhitaji wao".


Flaviana na Ujasiriamali
Mwanadada huyo mwembamba, mrefu, mcheshi na mwenye mvuto hajaishia tu katika kusaidia wanafunzi ila ameamua kuhakikisha kuwa anajikita katika ujasiliamali.


Ni siku mbili zilizopita Flaviana alizindua bodhaa zake za rangi ya kucha ziendazo kwa jina la Lavy. Lavy ni bidhaa za rangi ya kucha ambazo zipo kwa rangi mbalimbali.


Akizungumzia kuhusiana na bidhaa hiyo Flaviana anasema kuwa kwa upande wake ameamua kuanzisha biashara hiyo baada ya kuguswa na uhitaji wake katika soko.


Anasema kuwa bidhaa zake hizo zimelenga kuwasaidia watanzania kutumia bidhaa zenye ukaribu nao zaidi kwa kuwa bidhaa zake hizo za rangi ya kucha ni kwa ajili ya watanzania.


Anasema kuwa wazo la kuanzisha bidhaa hizo lilianza miaka miwili iliyopita ambapo alikuwa pia ana wazo na kuanzisha bidhaa za shule kwa wanafunzi.


Anasema kuwa baada ya kuona kuwa bidhaa za shule zimeshakuwa na mwelekeo na wanafunzi pamoja na wadau wengine wameshajua nini maana na umuhimu wa bidhaa zake hizo na kwa sasa anarejea kwenye lengo la rangi zake za kucha.


Kwa nini zinaitwa Levy
Jina la levy  kwa bidhaa zake hizo limetokana na jina lake yeye mwenyewe, Flaviana amekuwa akiitwa jina hilo na rafiki yake wa karibu kwa miaka mingi.


Rafiki yake huyo alikuwa akiunganisha jina la Flaviana Matata na kuamua kumita Levy jina ambalo hata yeye mwenyewe alipoanzisha biashara yake aliamua kutumia jina hilo.
Anasema kuwa kwa sasa anaona kuwa ni jina lenye thamani kuwa kwa kuwa kwanza lina mvuto na linaendana na uthamani wa bidhaa zake.


Anasema kuwa bidhaa hizo kuwa anaona kuwa haya akija kuamua kuanzisha bidhaa nyingine za urembo basi jina hilo ni jina ambalo linaweza kuwa mwafaka wabidhaa hizo.


Upatikanaji wake na bei
Flaviana anasema kuwa bidhaa hizo kwa sasa zinapatikana katika maduka ya Shear Illusion, Pikaso pamoja na Duka la Zuri ambapo anaongeza kuwa ni wakati mwafaka kwa watanzania kuanza kutumia bidhaa za nyumbani.


Anasema kuwa bei yake ni 5000/= na kuwa wanaweza kuzipata bidhaa hizo kila mara katika maduka hayo huku akisisitiza kuwa siku chache zijazo bidhaa hizo zitapatikana kila kona ya nchi.


Anasema kuwa kwa muda mrefu watanzania wamekuwa wakitumia bidhaa zenye nembo za watu maarufu wa Ulaya na Marekani na kuongeza kuwa ni muda sasa kuanza kutumia bidhaa zenye kuhasisiwa na watanzania wa hapa hapa nyumbani.


Anafafanua zaidi "najua watanzania wakiwekewa kitu bora na chenye kuwagusa na kuwafikia kirahisi basi wanakuwa na kila sababu ya kuunga mkono mtanzania mwenzao".
Flaviana na maisha yake binafsi


Mwanadada huyo ameolewa na kwa sasa yupo katika ndoa kwa miaka miwili, anasema kuwa akiwa kama mwanadada alielelewa katika mazingira ya kitanzania anajua maadili ya ndoa na anayatekeleza.


Anasema kuwa uanamitindo hauingiliani na maisha yake ya ndoa na kuongeza kuwa anaweza kutenga muda wake wa maisha ya ndoa na kazi yake ya mitindo.


Anasema kuwa mume wake ni mtu mwelewa sana na amekuwa msaada mkubwa katika maendeleo yake ya michezo na kuwa anajiskia amani na furaha kuwa na mumewe huyo.


Anasema kuwa yeye ni mwanadada ambae akiwa kwenye kazi anajua mazingira ya kazi na maadili yake na akiwa Tanzania anawahudumia wanafunzi anajua ni namna gani ya kufanya kazi nao.


Anaongeza kuwa kwa upande wake anajichukulia ni kama mwanadada ambae licha ya kuwa anajielewa ila anajiona ni mwenye majukumu mazito katika kusaidia maisha ya watanzania.


Anafafanua kuwa anafungua milango kwa wadau mbalimbali wanaotaka kujihusisha nae katika kuzungumzia jambo lolote kuhusiana na maendeleo ya kijamii na lolote ambalo linamguso kwa wananchi.


"Najua sisi kama watu maarufu wa hapa nchini tunajua nguvu yetu katika iliyopo kwenda kwa jamii, lakini je tunatumiwa kama inavyotakiwa mimi ninaona kuwa ninao ukaribu zaidi na wananchi na naweza kuwafikia kinachotakiwa kuwezeshwa ili kuwafikia wananchi" anasema Flaviana.


Ushirikiano wake na wadau wengine

Kwa upande wake mbunifu wa mavazi, Mgese Makory wa lebo ya Mgese Sisi anamzungumzia Flaviana kama ni mwanadada ambae anajituma na anajua ni kwa kiasi gani anatakiwa kushirikiana na wadau wengine wa fani ya mitindo na inayoendana.

Anasema kuwa amekuwa akimuona mwanadada huyo akijihusisha na masuala kadhaa kama vile kuhudhuria shughuli za wabunifu wengine wa mavazi, kutembelea miradi ya elimu kwa watoto pamoja na kuwa karibu na wanadada wenzake katika matukio mbalimbali.

"Mimi binafsi kama mbunifu wa mavazi na ndio nimebuni gauni lake alilovaa leo, najua ni kwa kiasi gani wanamitindo kama hawa na tena ambao wamekuwa kwenye ngazi za kimataifa wanavyokuwa ni vigumu kujitoa kwa watu ila kwa Flaviana amekuwa karibu na kila aina ya kundi la watu na kwa hilo hata bidha yake hii ya Levy ni lazima watu wataiunga mkono"anasema Mgese.

============

Related

Science 8208381997136466451

Post a Comment

emo-but-icon

item