Homecoming ya "Nape"kuoneshwa leo Sinema
http://habari5.blogspot.com/2016/01/homecoming-ya-napekuoneshwa-leo-sinema.html
Na Mwandishi Wetu
FILAMU ya Homecoming leo inaanza kuoneshwa kwa mara ya kwanza katika kumbi ya Sinema ya Mlimani City.
Filamu hiyo ilizinduliw a na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye mwezi uliopita ambapo aliisifia kutokana na ubora wake katika upigwaji wa picha, ujumbe, mahala ilipoigiziwa, mwongozo pamoja na mengineo mbalimbali.
Akizungumzia filamu hiyo mwongozaji wake, Seko Shamte alisema kuwa kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakiisubiria filamu hiyo na kwa sasa imeingia katika sinema.
Alisema kuwa itakuwa katika kumbi za sinema kwa muda wa wiki mbili na kuwataka wananchi kwenda kushuhudia filamu hiyo.
Alisema kuwa inahusiana na masuala kadhaa yahusuyo rushwa na mwenendo mzima wa matukio yaendanayo na rushwa na kuongeza kuwa ni wasaha kwa wananchi kujifunza na mambo mbalimbali kupitia filamu hiyo.
"Najua ni filamu ambayo imeandaliwa kwa ubora wa hali ya juu na sisi kama kampuni ya Alkamest Media iliyoandaa filamu hii tumelenga kuhakikisha kuwa tunafikisha ujumbe wa rushwa kwa vijana na jamii nzima ya kitanzania kwa staili ya kipekee ambayo ni kupitia filamu" anasema Seko.
Filamu hiyo imewashirikisha wasanii kama vile Daniel Kijo, Godliver Gordian, Magdalena Munisi, Issa Mbura, Ahmed Olotu (Mzee Chilo) Hashim Kambi pamoja na Doug Bramsen.
Kwa upande wake mwigizaji mkuu wa filamu hiyo Daniel Kijo amewataka watu kujitokeza kwa wingi kuiangalia filamu hiyo kwa kuwa kuna mengi ya kujifunza.