Tamasha la Pop Up Bongo chini ya udhamini wa Smirnoff lafana

Mratibu wa tamasha la Pop Up Bongo, Natasha Stambuli (kulia) akinunua bidhaa za duka la Chasing Fabulous wakati wa tamasha hilo, anaemuuzia ni Grolia Mwakasole na wa katikati ni Victoria Martin wamiliki wa duka hilo

Mmiliki wa duka beauty heaven Tanzania Winfrida Mgongolwa (kulia) akiwaonesha wateja waliotembelea eneo la duka lake katika tamasha la biashara la Pop Up Bongo lililofanyika Masaki juzi katika mgahawa wa Tuk Tuk Thai


Bidhaa kama hizi zilizotengenezwa kwa mbao zilikuwapo  pia
Na Mwandishi Wetu
MAMIA ya vijana walijitokeza juzi katika tamasha la biashara lililohusisha burudani ya muziki la Pop Up Bongo na kununua bidhaa mbalimbali.

Tamasha hilo la saba kufanyika kwa mwaka huu limefanyikia katika mgahawa wa Tuk Tuk Thai uliopo Masaki na kupambwa na burudani kutoka kwa Dj D Ommy.


Akizungumzia tamasha hilo, mratibu wake Natasha Stambuli alisema kuwa wabunifu wa ndani wengi wamejitokesha kushiriki tamasha hilo.


Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa na hamasa ya kubuni bidhaa zao wenyewe na kuziuza hasa wakihusisha zaidi nakshi za kiasili katika kupendezesha bidhaa hizo.


Alisema kuwa kutokana na mwamko huo tamasha hilo limewakutanisha wajasiriamali hao pamoja na wanunuzi kwa maana ya wateja ili wawaunge mkono.


Alisema kuwa bidhaa kama vile nguo, viatu vidani na bidha nyingine vimeuzwa katika tamasha hilo.
Alisema “kwa awamu hii ambayo ni ya saba tukiwa bado na mdhamini wetu kinywaji cha Smirnoff watu wengi wamejitokeza na kupata huduma kadhaa ambapo wamekuwa wakinunua bidhaa huku wakipata burudani ya muziki”.


Kwa upande wake Meneja wa vinywaji vikali kutokea, Serengeti Breweries Limited (SBL)  Shomari Shija alisema kuwa kampuni hiyo kupitia kinywaji chake cha Smirnoff imeamua kudhamini tamasha hilo kwa kuwa inatambua mchango wa ujasiriamali katika maendeoleo.


Mmoja kati ya wajasiliamali walioshiriki katika tamasha hilo, Sackry Papillon wa huduma ya mwili, The Rub Spa iliyopo Kijitonyama alisema kuwa tanmasha hilo limemkutanisha na wadau mbalimbali hasa vijana wanaopenda huduma hiyo.
===========

Related

Technology 4385867711168429849

Post a Comment

emo-but-icon

item