Pop Up Bongo kurindima kesho Masaki chini ya udhamini wa Smirnoff
http://habari5.blogspot.com/2016/04/pop-up-bongo-kurindima-kesho-masaki.html
Mratibu wa Tamasha hilo la Pop Up Bongo Natasha Stambuli akiwa katika tamasha hilo mwaka jana |
Hali ilivyokuwa mwaka jana katika tamasha hilo la Pop Up Bongo mwaka huu itakuwa ni bomba zaidi |
Tamasha hilo linalodhaminiwa na kinywaji cha Smirnoff kwa mwaka huu litashirikisha bidhaa kutokea Nyumbani Design, FT Boutique, Be More U, Beauty Heaven, Highsupsm, Zawadi Zambarau Gemstones and Kipilipili.
Akizungumza kuhusiana na tamasha hilo mratibu wake, Natasha Stambuli alisema kuwa kwa mwaka huu tamasha hilo litakuwa la aina yake likifanyikia mahala papya huku likiwa na bidhaa mbalimbali kutokea kwa wajasiliamali.
Alisema kuwa pia kutakuwa na burudani safi kutokea kwa Dj D Ommy ambae atatekeleza ile dhana ya biashara na muziki inayogusiwa katika tamasha hilo.
"Kwa kawaida hili tamasha limekuwa likifanyika pale Trinity Oyster bay lakini kwa mwaka huu linafanyika hapo Tuk Tuk Thai ambapo kuna eneo kubwa pia na litawavutia wengi" alisema Natasha.
Aliongeza kuwa " Pia burudani ya muziki itakuwapo ya nguvu kwa hiyo wananchi wajitokeze kwa wingi kwa kuwa kwanza ni bure kuingia na pia watapata kukutana na wauzaji wa bidhaa mbalimbali kwa hivyo watanunua na watacheza muziki pia".
Aliongeza kuwa kutakuwa na mauzo ya bidhaa kama vile nguo za wanawake na wanaume, viatu, nguo za asili, za watoto, bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi na hasa zile za kibunifu.
Alisema kuwa Pop Up Bongo imelenga kuwapatia nafasi wajasiriamali wadogo kukutana na kuuza bidhaa zao na hasa kuwekewa mazingira mazuri yanayowakutanisha na wateja kirahisi.
Alisema pia kuwa milango itakuwa wazi kuanzia saa nane mchana na shughuli itaendelea mpaka usiku na kutakuwa na ulinzi wa kutosha.
==========