Mkurugenzi
wa kampuni ya Mitindi ya Blackfox Modeling Agency Aj Mynah akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa utiaji wa saini wa makubaliano hayo pembeni ni
mwekezaji huyo David Johansson kutokea nchini Uingereza.
Na Mwandishi Wetu
FURSA kwa wanamitindo wa hapa nchini inaonekana kuanza kufunguka zaidi baada ya kampuni ya mitindo nchini Blackfox Modeling Agency kupata mwekezaji mpya kutokea nchini Uingereza.
Kampuni hiyo iliingia makubainao hayo na mwekezaji wake huyo hivi karibuni katika mgahawa wa Paparazi uliopo Sleep way ambapo mmiliki wa Blackfox Aj Mynah anasema kuwa hatua hiyo itafungua milango ya wanamitindo wa Tanzania nje ya nchi.
Alisema kuwa mkataba huo unalenga kuiongezea nguvu zaidi kampuni ya BlackFox katika harakati zake za kuiendeleza fani ya mitindo nchini na kuifanya kuwa ya kimataifa zaidi.
“Kama inavyofahamika kuwa fani hii ya mitindo nchini sio kongwe sana ikilinganishwa na nchi nyingine hivyo basi makubaliano haya yanalenga kuifikisha kampuni ya Blackfox kuwa ya kimataifa zaidi inayoweza kusaidia mamilioni ya vijana sio tu hapa nchini bali hata nje ya Tanzania” alisema Aj.
Aliongeza kuwa kampuni hiyo inalenga kufungua milango nchi nyingine za Afrika Mashariki, Afrika na hata kwenda katika nchi za Ulaya na Amerika.
Alisema kuwa kampuni hiyo imewandaa vijana wengi kuingia katika fani ya mitindo na kujiajili kama wanamitindo, matangazo na mengineo mengi.
Alisema kuwa chini ya mkataba huo wanamitindo wa hapa nchini wataweza kwenda kufanya kazi katika nchi za Ulaya na kwengineko.
Kwa upande wake mwekezaji huyo David Johansson alisema kuwa ameamua kuingia mkataba na Balck fox kutokana na fursa zilizopo hapa nchini kupitia fani hiyo.
Alisema kuwa Tanzania inao wadada na wakati kambao wanaweza kutangaza matangazo mbalimbali ya kimataifa na hata kufanya kazi nyingine zinazoendana na fani hiyo.
|