Makonda azindua nembo ya I love Dar, imeandaliwa na baa ya Element Oyster bay

Makonda akikata utepe kuzindua nembo hiyo
Hiyo ndio nembo ya I love Dar kama inavyoonekana
Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amezindua nembo ya I love Dar (naipenda Dar) inayobeba dhana nzima ya utalii wa ndani hususan mkoa wa Dar es Salaam.

Tukio hilo lilotokea juzi usiku majira ya saa saba huku likishuhudiwa na mamia ya watu waliojitokeza kwenye uzinduzi huo uliofanyikia katika baa ya Element iliyopo Oyster bay.

Akizungumza baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa nembo hiyo Makonda alisema kuwa ni hatua nzuri kwa wadau binafsi kujitokeza na kuendeleza mazuri kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema kuwa kwa kupitia nembo hiyo ya I love Dar inahamasisha kuendeleza uzuri wa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kutangaza kila aina ya kivutio chake.

Alisema, vipo vitu vya asili ambavyo vinatumiwa kama utalii hasa kuanzia majengo ya kizamani hasa maeneo na mjini, makumbusho za taifa zenye kuhifadhi historia ya Mkoa pamoja na mengineo.

Alisema kuwa nembo hiyo inaenda mbali hadi kuhamasisha masuala ya kimaendeleo ya Dar es Salaam likiwamo suala zima la usafi pia.

"Najua I Love Dar ni nembo ambayo inamaana kubwa sana kwa wananchi kwa ujumla kuipenda Dar ni pamoja na kufanya mazuri kwa ajili ya Mkoa huu hapo ikiwa ni suala zima la kutangaza vivutio, kuzingatia usafi na mengine yote mazuri" alisema Makonda.

Kwa upande wake  Meneja wa Baa ya Element, Mackenzie alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa inaunga mkono sera ya kuendeleza utalii wa ndani imeamua kuanzia kwa kubuni nembo hiyo.

Alisma hata katika majiji makubwa duniani kama vile New York ina nembo ya I love New York na kwa hapa nchini kuandika I love Dar ni mwanzo wa kuliendeleza jiji la Dar kwa kuanzia kwenye Utalii.

Related

Science 5287222747105635599

Post a Comment

emo-but-icon

item