Aliyogusia Kikwete katika hotuba yake ya kufunga mwaka
http://habari5.blogspot.com/2014/01/aliyogusia-kikwete-katika-hotuba-yake.html
Operesheni Kimbunga
Rais Kikwete alisema kukithiri kwa ujambazi katika mikoa ya Kigoma, Kagera na Mwanza ndiko kulimfanya akatoa uamuzi wa kuanzisha Operesheni Kimbunga ambayo imekuwa na mafanikio ya kutia moyo.
Alisema hali ya usalama katika Mikoa hiyo inaelekea kuimarika ingawaje ni mapema mno kusema tatizo limedhibitiwa. Lakini alikemea baadhi ya watu waliokuwa wanaishi nchini kinyume cha sheria kurudi kinyemela.
"Nimepata minong’ono kuwa baadhi ya watu walioondoka wanarudi kinyemela. Napenda kuwatahadharisha kuwa wasifanye hivyo. Wanajisumbua bure. Hawatadumu. Ushauri wangu kwao ni kuwa kama wanapenda kuishi Tanzania wafuate njia halali za kufanya hivyo," alisema.
Alisistiza kuwa uwajibikaji wa wana siasa peke yao hautoshi, kwani huwaacha waharibifu waendelee na kazi isivyostahili. Rais alisema mtindo huo utawafanya watumishi wasione umuhimu wa kutokurudia makosa.
Lakini alisema pale kwenye ushahidi wa wazi kwamba kiongozi wa kisiasa angeweza kuchukua hatua za kuzuia madhara lakini hakufanya hivyo lazima kiongozi huyo awajibike.
Upatikanaji wa chakula
Alisema kwa upande wa mazao ya chakula alisema nchi ilijitosheleza na akatoa mfano wa mwaka huu uzalishaji ulikuwa tani 14,383,845. Alisema ukilinganisha na mahitaji yetu ya chakula ya tani 12,149,120 hivyo nchi inajitosheleza na kuwa na ziada kidogo.
"Ziada hii ni kidogo hivyo inatulazimu mwaka ujao tuongeze maradufu juhudi na uwekezaji katika kutekeleza shabaha na malengo ya kilimo," alisema Rais Kikwete.
Usambazaji wa Umeme
Rais Kikwete alisema usambazaji umeme vijijini unaenda vizuri na akasema kutokana na kuongezewa fedha za bajeti, kasi ya usambazaji umeme imekuwa nzuri. Alisema tunaumaliza mwaka huku idadi ya Watanzania waliounganishiwa umeme ikiwa imefikia asilimia 24 ukilinganisha na asilimia 21 mwaka 2012 na asilimia 10 mwaka 2005.
Alisema hayo ni mafanikio kiasi na akaongeza kuwa kwa mwelekeo huo kufikia lengo la asilimia 30 ya Watanzania kupata umeme mwaka 2015 ni jambo la uhakika kabisa sasa. "Tena kuna uwezekano mkubwa wa kulivuka lengo hilo."
Msongamano wa Magari Dar
Rais alisema jitihada za kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam zimeendelea kutekelezwa. Alisema barabara kadhaa zilipanuliwa na kazi inaendelea ikiwemo ujenzi i wa njia ya kupita mabasi yaendayo haraka ambao ujenzi wake umeendelea kwa kasi ya kuridhisha.
Rais Kikwete alisema mchakato wa ujenzi wa barabara za juu ya nyingine katika njia panda za Tazara na Ubungo umeshaanza. Mwaka ujao huduma ya usafiri wa treni kusafirisha abiria Dar es Salaam itaongezwa ili watu wengi zaidi wanufaike.
uwekezaji
Rais Kikwee alisema hali ya uwekezaji sio nzuri hata kidogo kwa uchumi unaokusudiwa kujengwa kwa kutegemea uwekezaji wa sekta binafsi kutokana na mazingira ya uwekezaji nchini kutokuwa rafiki.
Alismea hivyo wanategemea Kitengo cha Rais cha ufuatiliaji wa miradi (PDB) kitatoa ushauri mzuri wa nini kifanyike kurekebisha hali hiyo.
ends