Bosi wa zamani TBS aanzia mwaka mahakamani






KESI ya matumizi mabaya ya madara na kulisababishia Shirika la Viwango nchini (TBS), hasara ya Sh milioni 68 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo Charles Ekelege, itasikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Jana kesi hiyo ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Augustino Mmbando kwaajili ya kuanza kusikilizwa, hata hivyo ilikwama kutokana na kukosekana kwa nyaraka halisi zilizotakiwa kutolewa kama sehemu ya ushahidi wa upande wa jamhuri.
Ekelege anadaiwa kusababisha hasara hiyo baada ya kuondoa ada ya asilimia 50 Kampuni za Jaffar Mohamed Ali na Quality Motors bila idhini ya Baraza la Utendaji kinyume na utaratibu wa TBS.

Awali Shahidi wa kwanza wa upande wa jamhuri, Mwanasheria wa TBS, Batista Bitao, alidai kuwa, kati ya Mwaka jana na mwaka huu alihusika katika kuhakiki nyaraka za uagizaji wa magari na barua za mawasiliano kati ya kampuni hizo na TBS, pamoja na muhtasari wa kikao cha wakurugenzi wa bodi.

Shahidi huyo aliomba nakala za nyaraka zipokelewe mahakamani kama sehemu ya ushahidi wake, upande wa utetezi ulipinga nakuiomba mahakama imuaru atoe nyaraka halisi na siyo nakala hata hivyo alishindwa kuziwasilisha na kesi hiyo kuahirishwa hadi leo itakapoendelea kusikilizwa.

Inadaiwa kuwa Machi 28, mwaka 2008 na Agosti 7, mwaka 2009 katika ofisi za TBS jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi Mkuu alitumia madaraka vibaya na kwa nia ovu alizipunguzia ada kampuni mbili kwa asilimia 50.

Ilidaiwa kuwa Ekelege aliziondolea kampuni hizo ada hiyo ambayo ni sawa na Sh milioni 68 bila idhini ya Baraza la Utendaji kinyume na utaratibu wa TBS.

Katika mashitaka mengine, Ekelege anadaiwa kuisababishia TBS hasara ya kiasi hicho cha fedha. Alikana mashitaka na yupo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti.
Mwisho.

Related

Sticky 1735230104770989055

Post a Comment

emo-but-icon

item