Naipongeza Yanga katika hili
http://habari5.blogspot.com/2014/01/naipongeza-yanga-katika-hili.html
WIKI hii Yanga ilienda kisiwani Zanzibar nakuonana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi kumwelezea sababu za kutoshiriki kombe la Mapainduzi.
Michuano ya kombe hilo ilianza Januari Mosi mwaka huu na Yanga ilijitoa ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
Sababu za Yanga kujitoa ilikuwa ni kutikana na kutokuwepo kwa benchi la ufundi ambapo wakati huo aliekuwa kocha mkuuwa timu hiyo Ernest Brandits alifukuzwa huku kocha msaidizi Fredy Minziro nae akipewa mkono wa shukrani na kwa nafasi yake kuchukuliwa na Charles Mkwasa huku ya kocha mkuu hadi sasa ipo wazi.
Yanga ilifanya mabadiliko hayo ya kulifuta benchi lake la ufundi kufuatia kufungwa 3-1 na Simba kwenye mchezo wa kuwania taji la Nani Mtani Jembe uliofanyika uwanja wa Taifa, Dar es salaa.
Yanga kwa kutambua kuwa kutoshiriki kwake katika kombe hilo ilipelekea pengo kubwa kwa mchuano hiyo iliamua kwenda kuomba radhi.
Mbali na kuomba radhi pia ilichangia milioni 10 kama sehemu yao ya mchango kwa michuano hiyo ambayo pia ni sehemu ya sherehe ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Binafsi naona kuwa Yanga ilifanya kitendo cha kiuungwana ambacho kinapaswa kuigwa na kupongezwa.
Yanga imetambua mchango wa Zanzibar katika kuimarisha klabu hiyo hasa ikizingatiwa kuwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar ndio alikuwa mwasisi wa klabu hiyo kongwe nchini.
Yanga kwa kutambua kuwa kitendo cha kutokuhudhuria sherehe hizo kilikuwa nje ya uwezo wao lakini wamegundua kuwa kuna fedha ambazo zimepotea na ambazo zingepatikana kwa njia ya mapato kama kiingilio wapo wangecheza.
Hivyo kwa kutoa milioni kumi kama sehemu ya fidia ina maanisha kuwa wamegundua hasara ambayo imepatikana na kuonesha urafiki na heshima kubwa wakaamua kwenda kisiwani humo kuomba radhi.
Uungwana kama huu ni mzuri hasa katika michezo kwa kuwa inarinda heshima ya klabu pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya klabu na serikali ya mapinduzi.
Ni vema Yanga ikaendelea kuwa na maamzi ya hekima kama haya kwa kuwa kwa kufanya hivyo ndio inazidi kujiongezea thamani kwa wanachama wake.
Katika kuonesha uwajibikaji Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji pamoja na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga walikuwa moja kati ya walioenda kuonana na uongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa sasa Yanga wapo nchini Uturuki na wanaendelea vema na mazoezi yao wakiwa chini ya Kocha Msaidizi Charles Mkwasa ambapo inajiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu utakaoanza January 25.
Yanga kwa sasa pia inamsaka kocha wake mkuu huku kukiwa na tetesi kuwa aliyekuwa kocha wa timu wa timu ya taifa, Taifa Stars Maxio Maximo ndio anakuja kukinoa kikosi hicho chenye makao yake makuu Jangwani