Kocha wa Simba ajibu Tambo za kocha wa Yanga
http://habari5.blogspot.com/2014/01/kocha-wa-simba-ajibu-tambo-za-kocha-wa.html
KUFUATIA tambo ambazo zimekuwa zikifanywa mara kwa mara na kocha mpya wa timu ya Yanga Hans Van Der Pluijm dhidi ya klabu ya Simba kocha wa Simba Zdravko Lugarusic amesisitiza kuwa bado timu yake itaendeleza ubabe kwa Yanga.
Hivi karibuni kocha huyo wa Yanga amekaririwa na vyombo vya habari akitoa kauli zinazoonesha kummudu kocha wa Simba kutokana na kuufahamu uwezo wake katika medai ya soka.
Kocha huyo katika kuoneshwa kuaminiwa zaidi na klabu yake juzi ilitangaza kumuongezea madaraka zaidi kwa kumpatia cheo cha Ukurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo.
Akizungumzia tambo za kocha huyo wa Yanga, kocha wa Simba Lugarusic alisema kuwa anatambua uwezo wa kufundisha alionao kocha huyo wa Yanga lakini bado sio tishio kwa timu yake ya Simba.
Aliongeza kuwa Simba itaendelea kuwa juu ya Yanga kwa kipindi chote kwa kuwa kikosi chake kina wachezaji wazuri na wenye kujiamini.
Aliongeza kuwa katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu utakaoanza hivi karibuni timu yake itafanya vema kutokana na walivyojipanga kufanya vema.
Aliongeza kuwa mchezo wa soka unapimwa uwanjani na wachezaji wa Simba wapo tayari kwa mzunguko huo utakaoanza Januari 25 mwaka huu.
Lakini hata hivyo alisisitiza kwa upande wake kuwa anamfahamu vilivyo kocha huyo, ana uwezo mzuri wa kufundisha.
"Huyu kocha ninamfahamu na ninatambua kazi zake kwa maana ya uwezo wake wa kufundisha lakini kwa Simba kocha huyu hatoweza kabisa kutuendesha"alisema Lugarusic.
Mwaka 2011 wakati kocha huyo wa Yanga akiwa anafundisha timu ya Berekum Chelsea, timu ambayo ilicheza na Ashanti Gold SC ya Ghana iliyokuwa chini ya Logarusic na alifanikiwa kushinda kwa 4-0 katika Ligi Kuu.
Hiyo imekuwa ikichukuliwa ni kama ujio wa kocha huyo katiak klabu ya Yanga ni kama ndio mwendelezo wa ubabe wa kocha huyo wa Yanga dhidi ya Logarusic wa Simba.
Yanga baada ya kufungwa 3-1 katika mchezo wa kuwania taji la Nani Mtani Jembe ililifuta benchi zima la ufundi la timu hiyo na kuajili kocha wake Mkuu wa sasa pamoja na msaidizi Charles Mkwasa.
Kwa sasa timu hiyo ipo Uturuki ambapo imeweka kambi kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu utakaoanza Januari 25 mwaka huu.
Mwisho