Kocha wa Yanga atua Uturuki
http://habari5.blogspot.com/2014/01/kocha-wa-yanga-atua-uturuki.html
Na Mwandishi Wetua
Kocha Mkuu mpya wa Young Africans Hans Van Der Plyum amewasili Uturuki na kujiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo nchini humo kwa wiki mbili ikijiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu.
Hans Van Der Plyum ambae ameingia mkataba wa kukinoa kikosi hicho kwa miezi sita kabla ya kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja iwapo akifanya vema.
Kocha huyo ambae alifanikiwa kuwaacha wenzake 52 walioomba nafasi hiyo na kwa sasa ameungana na timu hiy ambayo imekuwa chini ya kocha msaidizi Charles Mkwasa tangia kufukuzwa kwa benchi zima la ufundi la timu hiyo.
Akiwa katika jiji la Antlaya ambapo aliwasili jana kocha huyo anatarajiwa kutuma uelewa wake wa soka la Afrika katika kuhakikisha kuwa anakinoa kikosi hicho ambacho ndio kinashikiria ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya Yanga Abdallah Bin Kleb kocha huyo kwa sasa anaendelea na mipangilio yake ya mazoezi akiwa na timu yake hiyo.
Alisema kuwa sababu kubwa ya kumpeleka Uturuki ni kuungana na kikosi hicho na kuangalia namna ya kupanga safu nzima ya ushindi kwa kutumia wachezaji wake.
Alisema kuwa moja kati ya vitu ambavyo Yanga inatarajia ni kuona kocha huyo akiimarisha zaidi kikosi hicho na kujihakikishia ushindi wa michuano mbalimbali iliyopo mbele yao.
"Kikubwa ni kuona kuwa tunaendelea kufanya vema katika ligi kuu na Klabu Bingwa Afrika sasa kama inavyofahamika kuwa tuliona hatuna mwelekeo mzuri na tuliamua kufanya mabadiliko ya kumleta huyu"alisema Bin Kleb.
Aliongeza kuwa hata hivyo anakazi kubwa kwa kushirikiana na msaidizi wake Mkwasa kuhakikisha kuwa kunakuwa na mazingira mazuri ya nidhamu yatakayopelekea timu kuwa nzuri na yenye mwelekeo.
Mwishoni mwaka jana Yanga ililazimiak kulifuta benchi lake la ufundi kufuatia kufungwa 3-1 na Simba katika shindano la kuwania taji la Mtani Jembe.
Huenda ujio wa Mholanzi huyo ukarejesha imani ya wapenzi Yanga kwa timu yao hiyo hasa ikizingatiwa kuwa kocha huyo anaujua vema uwezo wa kocha wa Simba Zdravko Logarusic.
Mwaka 2011 akiwa anafundisha timu ya Berekum Chelsea timu yake ilikutana na Ashanti Gold SC ya Ghana katika mchezo wa Ligi Kuu na kuiadhibu 4-0.
Mwisho