Young Killer kurudi shule
http://habari5.blogspot.com/2014/01/young-killer-kurudi-shule.html
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Eric Msodoki maarufu kama Young Killer ambae kwa sasa anatamba na nyimbo zake kama vile Dear Gambe, Jana na Leo pamoja na Miss Super Star kwa sasa anajipanga kurudi tena shule.
Akizungumza na safu hii Young Killer alisema kuwa mbali na kuimba muziki na kupata mafaniko lakini anaona kuwa kwa sasa anatakiwa kujiendeleza tena.
Alisema kuwa akiwa kama msanii mdogo kiumri anahitaji kujipaga zaidi katika nyanja zote kuanzia muziki na hata za elimu pia.
"Kwa sasa nataka kurejea tena darasani kwa kuwa ndio kila kitu na sio kwamba nitakuwa siimbi hapana ila nitakuwa nafanya vyote kama kawaida napiga muziki na buku"alisema Young Killer.
Young Killer akiwa kama msanii mdogo kiumri amemaliza kiadto cha nne mwaka jana na kwa sasa ana mpango wa kusonga mbele.
Hatua hiyo ya Young Killer inaonekana kuwa itamtofautisha na wasanii wengine wenye umri mdogo ambao wana majina makubwa ambao wameishia kuimba na bile kujiendeleza kielimu.
================================