Makomandoo waja na ushaniloga
http://habari5.blogspot.com/2014/01/makomandoo-waja-na-ushaniloga.html
WASANII wa kundi la Makomandoo wametoa wimbo mpya uitwao ushaniloga.
Akizungumza na safu hii kiongozi wa kundi hilo Fred Wayne alisema kuwa katika wimbo huo ameshirikishwa msanii Quick Lacker.
Aliongeza kuwa kundi hilo limekuwa likitoa nyimbo mbalimbali nzuri na ambazo zimekuwa zikifanya vema sokoni.
Alisema kuwa wasanii wa kundi hilo wanatumia muda wao mwingi kutunga ikiwa pamoja na kuhakikisha kuwa wanafanya mazoezi kwa muda mrefu ili kutoa burudani safi.
Alisema kuwa kama ilivyo kwa nyimbo nyingine ambazo kila mojawapo ina staili yake ya kucheza ndiyo hivyo hivyo ilivyo kwa wimbo huo wa Ushaniloga.
Alisema kuwa wimbo huo utafanya vema kwa kuwa una maadhi kama ya nyimbo zao nyingine.
Alizitaja nyimbo hizo ni kama vile Kibega,Simama,Kibabababa, Ugonjwa wa Moyo na huo wa sasa uitwao Ushaniloga.
Kundi la Makomandoo linaundwa na wasanii kama vile Fred Wayne, Muki, G Clever, Suma L, Floor Master.
=================================