Mupili aomba msaada wa vifaa vya muziki

Na Mwandishi Wetu
MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa dansi nchini Kasim Mapili anaomba msaada wa vifaa vya muziki kwa ajili ya kuendelza vipaji vya wasanii wachanga.


Mapili ambae ni mmoja kati ya wanamuziki wakongwe nchini aliiambia safu hii kuwa ana shauku kubwa ya kuendeleza vipaji vichanga hapa nchini.


Alisema kuwa akiwa kama msanii mkongwe hawezi kuona kipaji chake kinapotea hivi hivi huku kukiwa na wasanii ambao wanahitaji msaada wake.


Alisema kuwa akipatiwa msaada wa vifaa vya bendi kama vila gitaa,ngoma,kinanda na vifaa vyingine muhimu atakuwa katika mazingira mazuri zaidi ya kufundisha vijana wengi


"Mimi ni mwanamuziki ambae ninajua kutumia kila aina ya kifaa cha muziki, kuanzia ngoma, kinanda na vinginevyo muhimu na ninahitaji sana vifaa hivi ili nitumie kuwafundishia watu kadhaa ili nao waufahamu muziki"alisema Mapili.


Aliongeza kuwa kwa sasa vijana wengi wameingia katika muziki huku wakiwa hawaujui muziki wenyewe unataka nini.


Aliongeza kuwa ili kuwa na muziki wa kitanzania inahitajika tijihada za ziada kama hizo za kuwaandaa wasanii chipukizi kwa kuwapatia elimu bora ya muziki zaidi.
====================================

Related

Sticky 6306062150862365999

Post a Comment

emo-but-icon

item