Yanga nao kulijadili suala la Okwi





KAMATI ya Usajili ya Klabu ya Yanga kukutana kwa ajili ya kujadili suala ya mchezaji wake Emanuel Okwi aliezuiliwa kucheza soka juzi.

Juzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya shirikisho iliyomzuia mchezaji kuendelea kuitumikia Yanga.


Akizungumza na gazeti hili Katibu Mkuu wa Yanga Bernard Njovu alisema kuwa Yanga inautaratibu wa kushirikiana na kamati yake ya usajili katika kila jambo kuhusiana na masuala ya usajili.


Alisema kuwa katika suala la Okwi kila kitu kilikuwa sawa na ndio maana kamati ya utendaji ililidhia kuingizwa kwa mchezaji huyo Jangwani.


Alisema kuwa kwa sasa wamesikia taarifa kuzuiwa mchezaji huyo kucheza kwa mshangao mkubwa na kuongeza kuwa hata hivyo hawajapewa taarifa maalum.


"Sisi tumesikia hili katika vyombo vya habari, hivyo hadi leo (jana) hatukuwa na taarifa rasmi kutoka kwa TFF kutuelezea kuzuiliwa kwa mchezaji huyu"alisema Njovu.


Alisema kuwa lakini hata hivyo wanawasiliana na TFF kuangalia uwezekano wa kupatiwa taarifa hiyo ili kujua ni nini hasa kinachitakiwa.


Alisema kuwa barua ndio inayotoa taarifa halisi kuhusiana na kile kinachotakiwa kufanywa kwa sasa na klabu hiyo.


Alisema kuwa huenda suala sio kuzuiliwa kwa Okwi kutokana na sababu zilizoelezwa kwenye vyombo vya habari labla kuna kitu kinachohitaji ufafanuzi zaidi.

Katika taarifa yake hiyo kwa vyombo vya habari TFF ilisisitiza kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.

Kamati hiyo ilibaini kuwa Okwi aliekuwa na  mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.

Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. 


Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.

Kufuatia hali hiyo TFF ndio iliamua kumzuia kwanza kuendelea kuichezea Yanga na kuandika barua kwenda FIFA yenye kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
Mwisho

   

Related

Sticky 3964761038822323948

Post a Comment

emo-but-icon

item