Wanaume saidieni kuepuka unyanyasaji wa kijinsia

a
WANAUME wametakiwa  kuyakemea  kwa nguvu  matukio ya ukatili wa kijinsia yanayowakumba zaidi wanawake na watoto nchini na  kutambua  kuwa vitendo hivyo vina madhara makubwa kiafya .
 

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki alisema hayo akiwa mkoani Pwani wakati akifungua warsha ya simku moja ya waandishi wa habari kuhusiana na sheria na sera zinazohusu ukatili wa kijinsia.
 

Ni warsha iliyondaliwa na Mradi wa Champion unaoratibiwa na shirika la Engenderhealth kwa lengo la kutoa uelewa kwa waandishi juu ya sera na sheria zinazohusu uktaili nchini.
 

Alisema wananchi wanahitaji kupata uelewa juu ya vitendo vya ukatili w akijinsia ili kwa wale wanaoathirika waweze kujua ni wapi watakapopata msaada wa kisheria.
 

Aliwataka kutambua umuhimu wa mradi huo  wanaume wanapaswa kuwa mabingwa wa kutokomeza vitendo hivyo ambavyo waathirika wakuu ni wanawake na watoto ambao hawajui kilio hicho kifike wapi ili waweze kusaidiwa.

“Waandishi andikeni kwa wingi kuhusiana na ukatili wa kijinsia ili wananchi wanaoathirika waweze kujua ni wapi wanapopeleka malalamiko yao…wanaume pia wajitokeze na kuwa mabingwa wa kudhibiti vitendo hivyo kama ilivyo maana ya mradi huo,” alisema Angellah na kuongeza kuwa asilimia 33 ya wanawake hufanyiwa vitendo hivyo nchini.


Pia aliomba waandishi nchini kuweka mikakati thabiti na endelevu ya kuripoti kikamilifu athari zinazotokana na sheria na sera kuhusu namna wahanga wanavyoweza kupata haki zao.

Kuhusu sera na sheria  alisema katika kupambana na ukatili wa kijinsia, sheria mbalimbali zilitungwa na zinatumika kuonesha msimamo wa serikali wakupinga ukatili wa kijinsia.
 

Naibu Mkurugenzi wa Engenderhealth, Dk. Monica Mhoja alisema ukatili wa kijinsia ni jamga kubwa ambapo mfumo dume uliojikita katika jamii umekuwa ukichangia sana.
 

"Kupitia mradi wa huo wanaume wanatakiw akuelimia ili kuwa chachu ya kuleta mabadiliko  katika suala la ukatili"alisema .
Mwisho.

Related

Sticky 6356317916514344258

Post a Comment

emo-but-icon

item