Bahari Rotary yawapokea waenda pikipiki kutokea Mombasa,

Wakiwa katika picha ya pamoja waendesha pikipiki hao pamoja na maofisa wa Bahari Rotary


Mr Jp akielekeza kitu kwa waendesha pikipiki hao


Kiongozi wao akizungumza na uongozi wa Bahari Rotary



Na Evance Ng'ingo
WAENDESHA Pikipiki wametakiwa kutumia kazi yao hiyo kuielimisha jamii katika kupambana na ugonjwa wa Polio.

Wito huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Chama Cha Waendesha Pikipiki wa Mombasa, Ally Fedha wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Fedha akiwa na waendesha pikipiki wenzake 20 wameendesha pikipiki zao wakitokea Mombasa nchini Kenya hadi Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kampeni yao katika kupambana na ugonjwa wa Polio.
Alisema kuwa waendesha pikipiki wanazunguka sehemu mbalimbali na wanakuwa wapo karibu zaidi ya wanajamii.

Alisema kuwa kwa kufanya hivyo wanaweza pia kutumia fani yao hiyo katika kuzungumza na wanajamii masuala mbalimbali kuhusiana na magonjwa na mambo mengineo ya kijamii.

"Najua uendeshaji wa pikipiki ni moja kati ya kazi za karibu zaidi na jamii, yani ni kazi ambapo mwendesha pikipiki anaweza kufika kila katika jamii inayomzunguka na kuzungumza na wanajamii husika tena kwa urahisi"alisema Fedha.

Akizungumzia harakati zao za kuhamasisha jamii dhidi ya ugonjwa wa Polio alisema kuwa wamezungumza na jamii za watu mbalimbali njiani wakiwa wanatokea Mombasa kuja Tanzania.
Alisema kuwa mbali na kufundisha na kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo pia wanachangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia klabu ya Mtwapa Rotary iliyopo Mombasa kupambana na ugonjwa huo.

Kwa upande wake Raisi wa Klabu ya Bahari Rotary ya hapa nchini, Ally Abdula alisema kuwa wamefurahishwa na juhudi za vijana hao kutokea Mombasa kuja hadi Tanzania kuelimisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Alisema kuwa klabu za Rotary ni klabu ambazo zipo kwa ajili ya wanajamii na zinahitaji pia kuwezeshwa ili kuihudumia jamii inayozizunguka.

"Hawa ni vijana ambao wameamua kuendesha pikipiki wakitokea Mombasa kuja hadi hapa nchini na njiani wamezungumza na watu mbalimbali na kuwaelimiesha namna bora ya kupambana na Polio sasa harakati kama hizi nzuri kwa kuwa pia wanachangisha fedha za kusaidia Klabu ya Mtwapa Rotary ya nchini kwao"alisema Abdula.

Waendesha Pikipiki hao waliwasili hapa nchini Ijumaa wakitokea Mombasa kupitia Tanga na kisha kuwasili Dar es salaam, na wanaondola leo hapa nchini.

=============== 

Related

Sticky 7299719498391546350

Post a Comment

emo-but-icon

item