Hebu msome Lil katika hili

MWANAMUZIKI wa Hip Hop wa Marekani, Lil Wayne, ameomba msamaha kwa kuchelewa kuachiwa kwa tape maalum yenye mkusanyiko wa nyimbo zake.

Ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu aachie tape yake hiyo lakini hata hivyo ilikuja kushindikana na kwa sasa itatoka mwishoni mwa mwezi huu.

Mwanamuziki huyo amekumbwa na matatizo makubwa katika kazi zake za sanaa kwa sasa ambapo moja kati yake ikiwa ni kuzuiliwa kutoka kwa albamu yake ya Cater V.

Alisema kuwa anatambua ni kwa kiasi gani anawakwaza wapenzi wa muziki wake ambao wamekuwa wakisubiria kusikia nyimbo nzuri kutoka kwake.

Alisema kuwa kwa miaka kumi ambayo amekuwa akitoa burudani amekuwa akiwakosha wapenzi wa muziki wake kwa hali na mali lakini kwa sasa anaona kuwa kuna vitu ambavyo vimekuwa vikiingilia ufanisi wa kazi zake.

"Ninaona kuwa ni kama ninakumbana na vitu ambayo kimsingi sikutakiwa kuwa navyo au kukutana navyo katika kazi yangu ya muziki hasa ikizingatiwa kwa muda ambao nipo kwenye hii fani". alisema msanii huyo.

Alisema kuwa amekuwa kwenye wakati mgumu katika ufanyaji wake wa kazi na wamilikiwa lebo ya Cash Money anayoitumikia.

Related

Sticky 6786015708861565485

Post a Comment

emo-but-icon

item