Tubadilishe sera ya kuwekeza kwenye nyumba-- Lamudi

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI pamoja na wadau wa sekta ya nyumba wameombwa kubadilisha kwa sera inayowazuia wawekezaji kutoka nje ya nchi kumiliki Ardhi, ili kuwapatia fursa wawekezaji hao kuwekeza kwenye sekta ya nyumba hapa nchini.

Wito huo ulitolewa jana Mkurugenzi Mkazi wa kampuni ya Lamudi, Godlove Nyagawa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mtazamo wa kampuni hiyo katika sekta ya nyuma kwa miaka 10 ijayo.

Alisema kuwa kwa upande wa kampuni yake hiyo ya kimataifa inayolenga  masoko ya juu ya mali zisizohamishika  yanayoibukia  kwa haraka- Lamudi, imebaini kuwa kuna dalili za kuwapo kwa ongezeko la riba kutoka kwa wawekezaji wa kimataifa ambapo pia biashara ya nyumba na makazi itahamia kidigitali zaidi.

Nyagawa, alisema kuwa katika tafiti zilizofanywa kwa njia ya mtandao na kampuni hiyo umebaini kuwa sekta ya nyumba itakua kwa asilimia 10.

Alisema kuwa zaidi ya asilimia 23 ya mawakala katika soko hilo wanaamini kuwa kutakuwa na ukuaji wa soko kwa asilimia kubwa na hivyo kuongeza thamani ya sekta hiyo.

Alisema kuwa kinachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kunakua na mabadiliko ya kisheria katika umiliki wa ardhi hasa nchi za kigeni.

"Katika masoko yanayoibukia kiuchumi, wageni hawana ruhusa ya kumiliki au kununua mali.  mfano katika nchi ya  Ufilipino, haikuwa na sheria ya kummilikisha ardhi mgeni , lakini katika mwaka  2015 mabadiliko ya kikatiba yanaweza kutokea"alisema Nyagawa.

Alisema kuwa kutakuwa na ongezeko kubwa la maslahi ya wawekeaji katika sekta hiyo ambapo wawekezaji wengi wameshaanza kujitokeza kuwekeza kwenye sekta hiyo hapa nchini.

Aliongeza kuwa "Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wawekezaji wa kigeni na riport kutoka Kituo cha Uwekezaji wa Nje (FDI) iliyofafanua kuwa kwa mwaka 2015 wawekezaji wanatarajiwa kuongezeka  na kuleta mabadiliko mengi Africa , hiyo pia ni ishara nzuri kwa mwaka huu kuwa na majengo mengi yene ubora  wa kisasa , kama inavyoonekana kwa maeneo  mengi  hapa Tanzania yameshakuwa miji kila siku zinavyongeeka

Aliongezea  kwa sasa Tanzania inatazamika ni kama nchi ya kati ambayo watu wake wengi ni wa tabaka la kati ikilinganishwa na wenye kipato cha juu na inatarajiwa kuwa kwa mwaka huu tabaka hilo litakuwa kiuchumi na litasababisha ongezeko la mahitaji ya nyumba.

Aliongeza kuwa kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la utafutwaji wa huduma za nyumba kwa njia za mtandao ambapo anatolea mfano wa tovuti yao ya Lamudi ambapo watu wengi hutumia mtandao huo kutafuta habari kuhusiana na nyumba.
==========


Related

Technology 2520635957979036170

Post a Comment

emo-but-icon

item