Yanga kuimalisha ushambuliaji

ishi Wetu
KOCHA wa Yanga Hans Van Pluijm  amesema kuwa anatumia siku zilizobakia kabla ya kukumbana na timu yaPolis Morogoro kuiandaa safu ya ushambuliaji.
Timu hizo zinakumbana keshokutwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ambapo kocha, Pluijm anasema kuwa utakuwa ni mchezo wa aina yake kwake.
Timu hiyo kwa sasa inafanyia mazoezi yake kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers uliopo Kawe ambao unaonekana kuwa ni uwanja wa kiwango cha chini ikilinganishwa na vile vya awali walipokuwa wakifanyia mazoezi.

Alisema kuwa ameona kuwa kuna tatizo kubwa katika sekta ya ushambuliaji kwenye timu hiyo na ameamua kuweka msisitizo kwenye sekta hiyo ili kuhakikisha kuwa wanaibuka na ushindi siku hiyo.
Alisema kuwa wachezaji wake washambuliaji wamekuwa wakishindwa kutumia vema nafasi wanazozipata kufanya mashambulizi kwa kuwa wanakuwa hawajiamini.
Alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakosesha ushindi katika michezo yao mingi na kuongeza kuwa kwa mchezo wao dhidi ya Polis Morogoro ndio itakuwa mwisho kwa hali hiyo kujitokeza.
"Washambuliaji ni watu muhimu tena sana kwenye mchezo wa aina yoyote kwa kuwa iwapo wakifanya vema na wakapata magoli basi kila mchezaji anakuwa na hamasa ya uchezaji na mwisho wa siku tunashinda"alisema mchezaji huyo.

Aliongeza kuwa " ataendelea na mafunzo kwa wachezaji wengine kulingana na uhitaji wa kila mchezaji huku akisisitiza kuwa mchezo wao dhidi ya Polis Morogoro utatoa picha halisi ya mafunzo atakayowafundisha".

Katika kuonesha ni kwa kiasi gani amejipanga na mchezo huo alisema kuwa ameamua kuwaandaa wachezaji wake wote kwa ujumla kujua ni kwa kiasi gani wanaweza kucheza kwenye mazingira magumu.

Alisema kuwa ameamua kuwafanyisha mazoezi kwenye uwanja huo ili kuanza kuuzoea uwanja wa Jamhuri mapema kwa kuwa nao pia ni uwanja uliopo kwenye hali mbaya.

Yanga ina pointi 15 ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
==========

Related

Sticky 8681256775388278276

Post a Comment

emo-but-icon

item